Rafael
Benitez, amesema kuwa atakihama klabu ya Chelsea mwezi Mei mwaka huu na kutaja
uamuzi wa kuumpa wadhifa wa kaimu kocha wa klabu hiyo kama kosa kubwa.
Akiongea baada ya kuongoza
Chelsea kushinda klabu ya Middlesbrough kwa magoli mawili kwa bila katika mechi
ya raundi ya tano ya kuwania kombe la FA, kocha huyo kutoka Uhispania, vile vile
aliwashutu mashabiki wa klabu hiyo.
Katika mahojiano na BBC, Benitez amesema
uamuzi wa Chelsea wa kuumpa cheo cha
kaimu kocha wa klabu hiyo ilikuwa kosa kwa
sababu yeye ndiye kocha mkuu kwa sasa.
Amesema mashabiki wao hawajawapa msaada
wanaohitaji na hivyo ameamua kuondoka mwisho wa msimu huu.'' Mashabiki sasa
hawana sababu ya kunung'unika kunihusu'' Alisema kocha huyo.
Mashabiki wa
Chelsea wakiwa na mabango ya kumtaka kocha huyo kufutwa kaziTangazo hilo la
kocha huyo wa zamani wa Liverpool limejiri baada ya baadhi ya mashabiki wa
klabu huyo kumdhihaki baada ya mechi yao na Middlesborough.
Kocha huyo mwenye
umri wa miaka 52, hajapata uungwaji mkono kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo
tangu alipoteuliwa kuchukua mahala pa Roberto Di Matteo mwezi Novemba mwaka
uliopita.
Katika mechi nyingi zilizopita za Chelsea, mashabiki wa klabu hiyo
hawakuficha hisia zao za kutaka kocha huyo kufutwa kazi.
No comments:
Post a Comment