UJIO wa Askari wa Shirika la
Upelelezi la Marekani (FBI) nchini na kuanza kufanya kazi, umewezesha kuanza
kunaswa kwa baadhi ya watu, wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya Padre Evarist
Mushi (55) wa Kanisa Katoliki Unguja, visiwani Zanzibar.
Akizungumza
katika mahojiano maalumu na Mwananchi Jumamosi Dar es Salaam jana,
Kamishna wa Polisi Zanzibar, Musa Ali Musa alithibitisha kwamba jeshi lake
limekuwa likishirikiana na FBI katika upelelezi huo na kwamba idadi ya
waliokamatwa imeongezeka.
“Ni kweli
tumekuwa tukishirikiana na FBI katika upelelezi ili kuhakikisha kuwa, wahusika
wa tukio la kuuawa kwa Padri Mushi wanakamatwa. Hii itasaidia kupunguza vitendo
vinavyohusishwa na matukio ya kigaidi yakiwamo mauaji,”alisema Kamishna Musa.
Alisema
kuwa hilo linafanyika ili kuhakikisha kuwa, zoezi la kuwakamata wahusika wa
uhalifu huo linafanikiwa kwa kiasi kikubwa, jambo alilosema linaweza kupunguza
matukio ya mauaji.
Alibainisha
kwamba hadi sasa kuna ongezeko la idadi ya watu waliokamatwa na kwamba watu hao
wanaendelea kuhojiwa, huku wengine wakishikiliwa kwa sababu maalumu.
Kamishna
Musa alifafanua kuwa kutokana na zoezi hilo watu watakaobainika kuhusika
na mauaji hayo watafikishwa kwenye vyombo vya sheria ili wachukuliwe hatua
zaidi.
Padri
Evaristus Mushi aliuawa Februari 17, mwaka huu kwa kupigwa risasi na watu
wasiojulikana waliokuwa katika pikipiki aina ya Vespa, wakati akienda kuongoza
misa katika Kanisa la Mtakatifu Theresia la Beit el Rass.
Juzi,
Kamishna Musa aliliambia Gazeti hili kwa njia ya simu kwamba wapelelezi wa
kigeni wamewasili Zanzibar kufanya uchunguzi wa kuwabaini waliomuua kwa kumpiga
risasi, Padri Evarist Mushi.
Alisema
kuwa wapelelezi hao tayari wameanza kazi hiyo kushirikiana na wenzao wa
Tanzania kuwasaka wauaji wa padri huyo aliyepigwa risasi Februari 17, mwaka
huu.
“Wapelelezi kutoka nje wamefika na wapo kazini,” alisema Kamishna Mussa bila ya kutaja wanatoka nchi gani.
“Wapelelezi kutoka nje wamefika na wapo kazini,” alisema Kamishna Mussa bila ya kutaja wanatoka nchi gani.
Pia
Kamishna Mussa hakutaka kueleza ni lini wapelelezi hao walifika Zanzibar na
idadi yao kwa maelezo kwamba hizo ni siri za polisi na kwamba zikivuja,
zitaingilia uchunguzi wanaoufanya.
Hata
hivyo, vyanzo vya ndani ya Serikali, vililithibitishia Mwananchi kuwa FBI
walikuwa wameanza kuwasaka wauaji wa Padri Mushi.
Kutua
kwa wapelelezi hao wa Marekani kunafuatia kauli iliyotolewa na Rais Jakaya
Kikwete katika salamu zake za rambirambi baada ya mauaji ya Padri Mushi, kuwa
amewaagiza polisi kutumia nguvu zake zote pamoja na kushirikiana na vyombo
vingine vya usalama vya ndani na mashirika ya upelelezi ya nchi rafiki katika
kufanya uchunguzi wa mauaji hayo.
Awali,
akitoa tamko la Serikali na kueleza kuwa Rais Kikwete ameidhinisha Serikali
kugharamia wapelelezi kutoka nje, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel
Nchimbi alihusisha tukio hilo na vitendo vya ugaidi.
No comments:
Post a Comment