Tangu kurudi kwake Nigeria, na kutengwa kuhudhuria mazishi ya anayedaiwa kuwa mpenzi wake, Goldoe Harvey nyota wa Big Brother toka nchini Kenya, John Makini anayejulikana zaidi kwa jina la Prezzo hajasema lolote kwa vyombo vya habari kuhusiana na majanga yaliyompata huko.
Prezzo, alikuwa Nigeria ambako alikwenda kwa ajili ya Sikukuu ya
Wapendanao na kukutana na kifo cha mshiriki mwenzake wa Big Brother na
mwanamuziki Mnaijeria, Goldie Harvey ambaye inaaminika walikuwa na uhusiano wa
kimapenzi.
Kilichokuja kuibuka na kumchanganya zaidi Prezzo ni mtu anayejulikana
kwa jina la Andrew Harvey ambaye aliachia mtandaoni picha za harusi yake na
mwanadada Goldie Harvey, ambaye pia siku chache zilizopita alionekana Nigeria
akihudhuria mazishi ya mwanadada huyo.
Prezzo kwa upande wake, aliwaambia wanahabari kwamba anahitaji muda wa
kupumzika kabla ya kusema lolote.
No comments:
Post a Comment