WAKATI kondomu feki zilizopigwa marufuku Uingereza mwaka jana
zikiwa katika mzunguko nchini Tanzania, kesi za gonjwa la ngono hatari
lisilotibika zimeongezeka kwa asilimia 25 Uingereza, huku wataalamu wakionya
kwamba ugonjwa huo umekuwa sugu zaidi katika tiba.
Zaidi ya kesi 21, 000 za maambukizi mapya zimedaiwa kutambulika kwa
mwaka 2011/12.
Kondomu hizo feki aina ya Trojan na Durex zenye vipele vipele ambazo
mwishoni mwa mwaka jana serikali ya Uingereza iliingia katika msako mkali
kusaka mamilioni ya kondomu hizo bandia zilizokuwa zikiuzwa nchini humo miezi
18 iliyopita.
Kirusi kinachoambukiza ugonjwa huo hatari kimetajwa kuwa ni 'Neisseria'
ambacho ni tofauti na vingine ambavyo mara nyingi hutibiwa kwa dozi moja tu
ya viuavijasumu (antibiotics) ambayo angalau hufanya kazi kwa asilimia 95
kiufanisi.
Akizungumzia maendeleo ya utafiti wa kondomu hizo nchini , Kaimu
Mkurugenzi wa Shirika la Wiwango Tanzania(TBS),Leandri Kinabo alisema
shirika hilo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Ckula na Dawa(TFDA) hivi sasa lipo
katika mchakato wa kuhakikisha vipimo halisi vya ubora wa bidhaa hizo
vinaangaliwa.
"Hili suala ni nyeti na ni la kiafya na usalama zaidi, hivyo
tulikaa kikao na TFDA na tulikubaliana tufanye uchunguzi wa kondom hizi, kwani
ni kweli zipo sokoni lakini suala la ubora linatakiwa kuangaliwa," alisema
Kinabo.
Aliwataka Watanzania kuwa na subira ili waweze kuchunguza bidhaa hizo
kwa umakini zaidi na kwamba baada ya uchunguzi watatoa majibu.
Baada ya gazeti hili kutaka kujua uhalali wa bidhaa hizo sokoni,
Kinabo alisema bidhaa zote zinazoingia bandarini hupimwa, lakini kuna baadhi ya
bidhaa ambazo huingizwa kwa njia zisizo halali na mara nyingi huwa feki.
"Inetegemea na lebo ya bidhaa husika, kuna wakati bidhaa inaweza
kupimwa na kuonekana kuwa ni salama na kisha kuingizwa sokoni, lakini baada ya
muda zikaingia bidhaa feki zenye nembo hiyohiyo, hivyo hilo ni suala la
kusubiri vipimo kutoka TFDA," alisema Kinabo.
Tatizo hilo sugu Uingereza limesababishwa kuanzishwa kwa kampeni mpya
ya kukabiliana na tishio kubwa la kuongezeka kwa kasi kwa magonjwa hayo nchini
Uingereza na Wales ambayo yamedaiwa kusambaa kwa wingi nchini humo na nchi
zinazoendelea.
Wataalamu wa Afya wana matumaini mapya baada ya kuanzishwa mpango
mkakati wa kuzuia ugonjwa wa gono 'Gonorrhoea Resistance Action Plan' ambayo
itaongeza ufahamu wa ugonjwa huo.
Mpango huo ulioanzishwa na shirika la Ulinzi wa Afya, utafuatilia
tatizo hilo la kimataifa linaloongezeka kwa kasi tangu kupungua miaka 10 iliyopita.
No comments:
Post a Comment