Rais wa Kenya Mwai Kibaki anayehudumu muhula wake wa wisho , amewataka wakenya kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kwa njia huru na ya haki watakapokwenda kwenye debe Jumatatu.
Amesema kuwa wakenya watakuwa wanaandika historia ya nchi kwa kushiriki
katika uchaguzi siku hiyo. Akihutubia taifa kwa kupitia kwa televisheni ya
taifa, Kibaki pia alisema kuwa serikali imehakikisha kuwa imedhibiti usalama
kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kwa amani.Aidha amewataka wagombea
kukubali matokeo ikiwa watashindwa wakati akiwataka washindi kuwa wanyeyekevu
katika kupokea ushindi.Kibaki aliapishwa kwa muhula wa pili tarehe 30 mwezi
Disemba mwaka 2007 baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata mkubwa kiasi cha
kusababisha maafa huku maelfu wakiachwa bila makao hadi leo.Serikali ya Muungano
iliundwa baadaye kama hatua ya kutuliza ghasia huku makubaliano yakitiwa saini
ambapo Raila Odinga aliyekuwa mpinzani wake mkali akipewa wadhifa wa waziri
mkuu.
No comments:
Post a Comment