Rais wa
Marekani Barack Obama, ni miongoni mwa viongozi wa dunia walioalikwa kwa
sherehe za kumuapisha rais wa nne wa Kenya.
Mkuu wa utumishi wa
umma, Francis Kimemia amesema kuwa serikali imewaalika Waziri mkuu wa Uingereza
David Cameron na marais wa nchi za Muungano wa Ulaya.
Pamoja na walioalikwa , ni
marais wa kanda ya Afrika Mashariki.Rais wa Uganda Yoweri Museveni,Jakaya
Kikwete wa Tanzania , Paul Kagame wa Rwanda na Rais wa Burundi Pierre
Nkurunziza.
"Mnaweza kuwa na uhakika kuwa tutamwalika rais wa Marekani,
kushuhudia sherehe za kuapishwa kwa rais mpya,'' alisema Kimemia kwenye mkutano
wa waandishi wa habari.
Bwana Kimemia aliwataka wakenya kupiga kura kwa amani
wakati wa uchaguzi huo.
"tunawataka wakenya kuweka amani. Sisi tumefanya
mikakati ya kuhakikisha kutakuwa na usalama wa kutosha na kuhakikisha kuwa
tutafaulu,'' aliongeza Kimemia.
Rais mpya anatarajiwa kuapishwa tarehe 26, mwezi
Machi, wiki tatu baada ya wakenya kumchagua.
Hata hivyo, hili litafanyika tu
ikiwa kutakuwa na mshindi bayana na kuzuia duru ya pili ya uchaguzi.Mgombea
anastahili kupata zaidi ya asilimia hamsini ya kura zote na angalau asilimia 25
katika nusu ya kauti zote nchini.
No comments:
Post a Comment