Mapigano ya wapiganaji wa kiislamu na vikosi vya usalama nchini Nigeria
yameripotiwa kutokea tangu usiku wa Ijumaa na kuendelea kwa muda mrefu ambapo
jumla ya watu 185 wanaripotiwa kufariki dunia katika mapigano hayo yaliyotokea
Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Serikali ya mji wa Baga na
Ofisa Serikali hiyo Bwana Lawan Kole.
Inasemekana kuwa watu wengi zaidi wamefariki dunia ambapo bado juhudi
za kutafuta maiti nyingine zinaendelea. Brigedia Jenarali Austin Edokpaye
amewaambia maafisa wakuu wa serikali kuwa,wapiganaji walitumia silaha kali na
maroketi yenye mabomu mazito kupambana na vikosi vya jeshi.
Aidha bwana Edokpaye aliongeza kuwa,wapiganaji hao walikuwa wakitumia
raia kama kinga yao kwa kujibanza karibu na makazi ya watu ambapo walijua vikosi
vya jeshi visingeweza kujibu mapigo.
Nigeria imekuwa ikikabiliwa na vifo vya raia wengi tangu kuibuka kwa
vikundi vya wapiganaji wa kiislamu mwaka 2010 ambapo vingi vimejikita Kaskazini
mwa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment