Language

Wednesday, 16 January 2013

HABARI: OLE WAKE ATAKAEICHEZEA SERIKALI

Serikali imesema haitavumilia kwa namna yeyote ile vurugu za kidini, kikanda na ukabila ambazo baadhi yake zilitaka kulitia doa taifa mwaka jana.

Pia imesisitiza kwamba haitawavumilia wanasiasa wanaotumia rasilimali za taifa kujitafutia umaarufu kwa gharama za kuligawa taifa.
Akizungumza na mabalozi kwa nyakati tofauti Ikulu, Dar es Salaam; kwanza katika sherehe ya kuukaribisha Mwaka Mpya iliyofanyika juzi na alipokuwa akiagana na Balozi wa Uingereza nchini, Dianne Corner jana, Rais Jakaya Kikwete alisema vurugu zilizotaka kujitokeza mwaka jana zinatosha.
Serikali haitavumilia vurugu wala ukabila kwa namna yoyote ile…. Mwaka 2012 vurugu zenye sura ya kidini zilianza kujitokeza ila sasa nasema kwamba hatutazivumilia kwa namna yeyote ile, inatosha,” alisema Rais Kikwete.
Akizungumza katika hafla hiyo, Kiongozi wa Mabalozi ambaye pia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Juma Mpango alisema jumuiya ya mabalozi imefurahishwa na namna ambavyo Serikali imekuwa ikishughulikia vurugu za kidini ambazo zilitaka kujitokeza bila kusababisha madhara kwa wananchi.
Tumeridhishwa na namna ambavyo Serikali imekuwa inashughulikia mambo yake vizuri. Tunaomba mwendelee kushughulikia amani ya nchi hii maana ndiyo mhimili wa nchi za Maziwa Makuu,” alisema Balozi Mpango.

Kuhusu gesi
Rais Kikwete alizungumzia suala la rasilimali za taifa na kusisitiza kuwa pia hatavumilia kuona wanasiasa wakitumia suala la gesi kujitafutia umaarufu.
Wakati Rais Kikwete akitoa kauli hiyo jana, habari kutoka Mtwara zilidai kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amewekewa magogo barabarani kumzuia asiende kwenye kijiji kinachozalisha gesi hiyo, huku Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo akizomewa.
Hata hivyo, polisi walikiri wananchi kuweka magogo barabarani kwa lengo la kumzuia waziri huyo, lakini ikaeleza kuwa gari lililozuiwa siyo la Simbachawene.
Akizungumza na Balozi Corner, Rais Kikwete alikemea tabia ya baadhi ya viongozi wa kisiasa kutumia suala la rasilimali za taifa, ikiwamo gesi asilia kujitafutia umaarufu wa kisiasa na kuwapotosha wananchi.
Ni jambo la hatari na lisilo na tija kwa wanasiasa kujaribu kuigawa nchi vipandevipande kwa sababu ya kujitafutia umaarufu kwa kutumia rasilimali za taifa,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:
Unawezaje kuwa na nchi moja na taifa moja wakati kila mmoja anadai rasilimali kutoka kwenye eneo moja ibakie na kunufaisha watu wa eneo hilo tu. Huwezi kuwa na nchi moja na yenye umoja wakati kuna nchi ya gesi asilia kule Mtwara, kuna nchi ya kahawa kule Kilimanjaro, kuna nchi ya chai na ndizi kule Bukoba,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:
Kwa sababu kama gesi asilia inatakiwa kubakia na kunufaisha watu wa Mtwara tu, basi wenye haki zaidi ya kudai jambo hili siyo watu wa Mtwara, bali ni watu wa Msimbati ambako ndiko ilipogunduliwa gesi ambako ni maili 60 kutoka Mtwara, kilomita 200 kutoka Newala.

Tuesday, 15 January 2013

HABARI PICHA: NDOA ZA JINSIA MOJA ZINAZIDI KUSHIKA KASI AFRIKA


HABARI: KIGOGO WA CCM MSAGAJI HUYU HAPA

Mwenyekiti wa CCM, Tawi la Washington DC, Marekani, Loveness Mamuya, yupo kwenye uhasama mkali na Mtanzania mwenzake anayeishi nchini humo, Linda Bezuidenhout, kiasi cha kuchafuana na kuibua aibu nzito.

Loveness

Rekodi zinaonesha kuwa Loveness na Linda walikuwa marafiki wakubwa lakini kwa sasa ni maadui wasiopikika chungu kimoja, huku mitandao ya kijamii, hususan Facebook na skendo ya usagaji, vikitajatajwa katika malumbano yao.
Baada ya malumbano na kuchafuana, wiki iliyopita mwandishi wetu aliwapata mahasimu hao, akarekodi sauti zao ambapo kila mmoja alitoa ya moyoni kuhusu mwenzake.
ALICHOKISEMA LINDA

Linda

Linda ambaye ni dada wa mshindi wa Big Brother Africa mwaka 2007, Richard Bezuidenhout alidai: “Tatizo kubwa la Loveness ni usagaji. Miaka saba iliyopita wakati naishi Maryland (Marekani), nilikuwa na matatizo ya nyumba. Nilikuwa sina hati za kuniwezesha kupanga nyumba yangu mwenyewe.
“Nikawa nachangia nyumba na watu wa nchi nyingine, nanyanyasika, tunagombana. Loveness akasikia matatizo yangu, akanipigia simu. Akaniambia ananijua tangu nikiwa Dar es Salaam. Baadaye akanishawishi nihamie kwake halafu atanisaidia kupata hati niweze kupata nyumba niishi mwenyewe na watoto wangu. Wakati huo nilikuwa na watoto wawili, mmoja ana miaka sita, mwingine mmoja na nusu.
“Nilipohamia nyumbani kwake, siku zikawa zinakwenda hafuatilii makaratasi yangu wala hataki kujishughulisha kunitafutia nyumba. Kinyume chake akawa ananitongoza tusagane, mimi nikamkatalia, basi akawa ananifuata chumbani usiku, ananilazimisha tufanye huo mchezo wa kusagana.
“Kila siku alikuja chumbani kwangu, mimi nikawa nashindwa kumjibu kwa ukali kwa kuhofia atanifukuza, nikawa nasingizia watoto wangu hawajalala, yeye anasema wamelala, mimi naendelea kumsisitizia hawajalala kwa sababu mimi ndiye nawajua.
“Siku zikawa zinakwenda, siku moja nikamuuliza ni kwa nini hataki kunisaidia kupata nyumba, au mpaka anifanyie huo mchezo? Hapo nikawa nimemtibua lakini baadaye ikabidi nijifanye nimelainika, akatulia lakini nikaendelea kumkatalia kijanja kunifanyia huo mchezo wake.
“Kuna wakati alinunua mpaka nyeti bandia ya kiume akidhani mimi nitakubali. Vilevile kuna siku alinibaka, hiyo siku siku alinunua pombe tukalewa, nilipolala, katikati ya usingizi nikashtuka kusikia mtu amenilalia.

“Nikamsukuma, kutokana na pombe sikumzingatia, nikaendelea kulala. Asubuhi nikakumbuka lile tukio, nikamuuliza Loveness kama alikuja chumbani kwangu usiku, akanijibu ndiyo na nilimsukuma. Akaniambia pia kwamba hakutaka kuendelea kwa sababu aliponishika aligundua nilikuwa katika siku mbaya.
“Nikajua mambo yamekuwa mazito, kwa hiyo nikamuomba anisaidie kupata nyumba, baada ya hapo, atakuwa anakuja kwangu tunafanya huo mchezo kwa kujiachia. Kusikia hivyo, Loveness akaondoka na mume wake, wakaenda kutafuta nyumba, jioni wakaniambia wamepata.
“Yaani baada ya kumuahidi tutakuwa tunafanya mchezo wake ndiyo akapata nyumba haraka. Nikahamia na watoto wangu. Baada ya hapo, nikamhamishia na mdogo wangu mwingine. Loveness akaona mdogo wangu atakuwa anamfanya asifanikiwe lengo lake la kufanya mchezo wa usagaji na mimi.
“Loveness akanigombanisha na mdogo wangu, akahama lakini baadaye yule mdogo wangu akaja kunipa siri nzima ya maneno ya uchonganishi aliyokuwa anaambiwa na Loveness. Kwa kweli kitendo cha kunigombanisha na mdogo wangu kiliniudhi sana, ikabidi nianike uchafu wote na njama zake za kujidai ananisaidia ili anifanyie mchezo wa usagaji.”

 

LOVENESS NAYE AKAZUNGUMZA
“Mimi Linda alikuwa rafiki yangu, alibadilika tu kwa sababu ya kunionea wivu. Ni uongo mtupu,” alisema Loveness na kuongeza:
“Kiukweli tuligombana kwa vitu tofauti. Alikuwa anaishi kwangu nikamfukuza kutokana na tabia zake lakini nashangaa haya mambo yamekua makubwa hivi sasa.”
SIASA ZATAJWA
Loveness: “Mimi naamini haya maneno ya Linda yamechochewa na siasa. Unajua tangu tufungue tawi la CCM DC, imekuwa tabu sana. Maneno mengi yanazungumzwa. Mfano, mimi na Linda tuligombana karibu miaka saba iliyopita lakini hayakusemwa, nilipofungua tawi la CCM tu ndiyo mambo yakawa makubwa.
“Wakaanzisha mpaka ukurasa wa kikundi Facebook, wakawa wananitukana. Mimi sishangai sana kwa maana Linda ni Chadema damu na mimi ni CCM damu, hizi ni siasa tu.”

BURUDANI: HIZI NDIO PICHA ZILIZOACHA MASWALI KWA WATU 'BAADA YA DIAMOND NI ZAMU YA JB KWA WEMA???'



HABARI: UN YAUNGA MKONO MAJESHI YA UFARANSA MALI

Wanachama wote wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wameunga mkono harakati za jeshi la Ufaransa dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu nchini Mali.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon alisema kuwa anatumai hatua ya jeshi hilo itaweza kurejesha utulivu na uthabiti nchini humo.
Ufaransa iliingilia mzozo huo siku ya Ijumaa baada ya wapiganaji kuanza kusonga mbele Kusini mwa nchi.
Maafisa wa utawala nchini Ufaransa, walisema kuwa wanahofia waasi huenda wakaukaribia mji mkuu Bamako na kusababisha tisho kubwa la usalama katika eneo hilo zima.
Siku ya Jumatatu , baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, lilifanya mkutano mjini New York kufuatia ombi la Ufaransa.
Baada ya mkutano, balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa,Gerard Araud alisema kuwa nchi yake inaungwa mkono na wanachama wote wa baraza la usalama.
Lakini aliongeza kuwa Ufaransa pia ilitaka wanajeshi wa nchi za Afrika Magharibi kupelekwa Mali mara moja.
Hatua ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuunga mkono jeshi la Ufaransa ni ishara ya wasiwasi mkubwa uliopo kuhusu uwezo wa makundi ya kiisilamu yaliyojihami nchini Mali.
Wanadiplomasia wanaonekana kuwa na wasiwasi kuhusu kuwasili kwa wanajeshi nchini Mali kusaidia na harakati za jeshi la Mali dhidi ya waasi.

MITINDO: KAMA UNAPENDA KUTUPIA SUIT (SUTI) HII INAKUHUSU ZAIDI








BURUDANI: KAMA ULIKUWA HUJUI LEO NI BIRTHDAY YA PITBULL, NA HIKI NDICHO ALICHO KITWEET KUTOA BAADA YA KUPEWA SALAMU ZA BIRTHDAY YAKE

Born: January 15, 1981 (age 32), Miami
Height: 1.77 m
Full name: Armando Christian Pérez
Nationality: American


MICHEZO: HII NDIO MECHI YA KESHO KATIKA LIGI KUU UINGEREZA


Monday, 14 January 2013

HABARI: VIFO VYA MAMA NA MTOTO SAS BASI


MAKAMU wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, leo anafungua mkutano wa kimataifa wa Afya ya Mama ambao utahusisha washiriki kutoka zaidi ya nchi 68 wakiwemo wanasiasa.


Akizungumza na waandishi wa habari mjini Arusha jana, Mkurugenzi wa Asasi ya Management and Development for Health (MDH), Dkt. Chalamila Guerino, alisema mkutano huo utakuwa na manufaa kwa afya ya wanawake wajawazito ambao kila siku wanapoteza maisha wakati wa kujifungua.Alisema mkutano huo utakuwa wa siku tatu, utajadili changamoto mbalimbali wanazopata wajawazito kwenye uzazi na utafungwa Januari 17 mwaka huu na Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete.“Mkutanio huu utakuwa na washiriki wasiopungua 700, wakiwemo wanasiasa ambao watapewa mbinu mbalimbali zitakazowasaidia kujua masuala ya afya ya mama ili kupunguza vifo vinavyotokea.“Wanasiasa watapewa mbinu na elimu ya kuzungumza na wananchi ili jamii iweze kuepukana na vifo vinavyochangia umaskini nchini,” alisema Dkt. Guerino.Akizungumzia vifo vya wajawazito hasa wakati wa kujifungua, alisema Tanzania bado inakabiliwa na changamoto hasa maeneo ya mijini ambayo vifo ni vingi.“Takwimu za kidunia nazo zinaonesha kuwa, asilimia kubwa ya wanawake wanapoteza maisha hasa wakati wa kujifungua, nchini Tanzania wanawake 454, kati ya 100,000 hufariki dunia wakati wa uzazi huku.“Kwa nchi zinaendelea duniani, wanawake 300,000 hufariki dunia hivyo tunapaswa kupambana na hali hii haraka kwa kuhusisha makundi mbalimbali pamoja na wanasiasa,” alisema.Alisema kwa upande wa mijini nchini, changamoto bado ni nyingi ambapo ili vifo hivyo viweze kuwa historia, lazima tuwe na umoja ambao ni thabiti ili kuokoa maisha ya wanawake.Aliongeza kuwa, mkutano huo pia utajadili upatikanaji wa vitendea kazi ili kuboresha huduma ya afya kwa wajawazito na upimaji ubora ambapo kupitia mada hizo, Tanzania itaweza kuepusha vifo vingi vya wanawake wajawazito.

BURUDANI: JOKATE 'KIDOTI' KUOLEWA MWAKA HUU?

Miss Temeke 2006/07, Jokate Mwegelo 'Kidoti' anadaiwa kuchumbiwa kwa siri nyumbani kwao, Songea mkoani Ruvuma alipokwenda kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa staa huyo, Jokate alitimba Songea akiongozana na rafiki zake wawili pamoja na baadhi ya ndugu.
Chanzo hicho kilidai kuwa kilipochunguza amekwenda kufanya nini mkoani humo, ndipo ikabainika kuwa alikwenda kusherehekea Mwaka Mpya akiongozana na wazazi wake anaoishi nao Dar, lengo likiwa kukamilisha mambo ya mila kwani alikuwa ameposwa na mchumba ambaye hakutajwa.
Mtu huyo aliendelea kudai kuwa nyumbani kwa akina Jokate ambaye aliapa kuwa lazima mwaka huu aolewe, kulikuwa na wageni wengi ambao miongoni mwao ndiyo waliopeleka posa.
Baada ya habari hizi kutua mezani,mwandishi wetu aliongea na Jokate kwa njia ya simu ambaye alikiri kwenda kwao Songea lakini hakutaka kudadavua ishu ya kuchumbiwa.
“Mh! Watu ni wambeya jamani! Mimi nilienda kwetu na ninatarajia kufanya kitu kikubwa huko Songea mtakisikia ‘soon’,” alisema Jokate huku akicheka.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...