Vichwa Vya Habari
Language
Wednesday, 13 February 2013
HABARI MUHIMU-OLE WAO WANAWAKE WAVUTAJI WA SIGARA
Wataalamu wa afya wanasema kuwa wanawake barani Ulaya wanafariki zaidi kutokana na saratani ya mapafu kuliko saratani ya matiti.
Wanaelezea kuwa saratani ya mapafu ndio imekuwa sasa saratani nambari moja ambayo inasababisha vifo miongoni mwa wanawake.
Hali hii tayari inashuhidiwa nchini Uingereza na Poland.
Kulingana na watafiti, hii ni ishara ya idadi kubwa ya wanawake wanaovuta sigara hali iliyoanza kujitokeza kuanzia mapema miaka ya tisini na sabaini.
Idadi ya vifo vinavyotokana na saratani ya mapafu, vitaendelea kuongezeka katika miaka ijayo, lakini sasa kwa sababu ya vijana wa kike wasiovutiwa na kuvuta sigara na ambao idadi yao sio kubwa sana , huenda vifo hivyo vikapungua.
Mwaka 2013, takriban wanawake 82,640 barani Ulaya watafariki kutokana na saratani ya mapafu ikilinganishwa na wanawake 88,886 watakaofariki kutokana na saratani ya matiti.
Wanatarajiwa kuwa vifo vinvyotokana na saratani ya mapafu kupungua mwaka 2020 au 2025 kwa sababu angalu vijana wa kiike hawavuti sana sigara.
Lakini ifikapo mwaka 2015, wanawake wengi watafariki kutokana na saratani ya mapafu kuliko saratani ya matiti, kulingana na mtaalamu wa afya ya wanawake, Profesa Carlo La Vecchia .
Takwimu zinaonyesha kuwa ingawa watu wengi zaidi wanaugua saratani, kwa sababu wanaishi muda mrefu zaidi,
ni watu wachache sana wanafariki kutokana na saratani.
Licha ya kupungua kwa idadi ya watu wanaofariki kutokana na saratani barani humo, idadi ya wanawakewanaofariki kutokana na saratani ya mapafu inaongezeka katika nchi zote za Ulaya.
Profesa La Vecchia,wa chuo kikuu cha Milan, Italy, anasema kuwa hali hii inaleta wasiwasi kwa sababu hakuna dalili kuwa ugonjwa huo unapungua.
Uvutaji sigara pamoja na ugonjwa wa sukari ndio vinachangia kuongezeka kwa ugonjwa huu. Lakini wataalamu wanasema bado hawajui nini kinasababisha sehemu kubwa ya saratani hiyo.
Wataalamu wanasema kuna umuhimu wa wanawake kuwacha kuvuta sigara
BURUDANI: N'SYNC-THIS I PROMISE LYRICS
"This I Promise You"
Ohh ohh...
When the visions around you,
Bring tears to your eyes
And all that surround you,
Are secrets and lies
I'll be your strength,
I'll give you hope,
When the visions around you,
Bring tears to your eyes
And all that surround you,
Are secrets and lies
I'll be your strength,
I'll give you hope,
BURUDANI: TID NAYE KWENDA BIG BROTHER AFRICA
Baada ya jana kusikia kuwa q
chifu kachukua form TID nayeye naye kachukua form ya kushiriki big brother na kufiksha idadi ya wasanii wa ongo
kuwekahistoria ya kuchukua form za big brother ambako wema sepetu na nyeye
aliichukua q cheaf na hemed pia wato kwenye nia ya kubeba kitita cha dola za
kimarekani 300,000
Mshiriki wa mwaka jana Julio aliongea
nakusema mtu kama TID angefaa sana kushiriki shindano hilo maana ni mcheshi na
ana vigezo vingi vitavyomuwezesha kushinda.
BURUDANI: KUNDI LA MUZIKI LA PAH ONE LAMONG'ONYOKA!!!
Kundi ambalo
lilikuwa linaundwa wasanii wanne kwa pamoja likiitwa Pah One sasa limevunjika
kwani First Lady
wa kundi hilo la Pah One
mwanadada Aika
ametangaza kujitoa rasmi kwenye kundi hilo pamoja na rapper na producer wa
kundi hilo Nahreel
na hivyo kundi hilo kubakiwa na wasanii wawili tu.
Aika amesema kuwa sababu ya
kumfanya ajitoe kwenye kundi hilo ni kutokuwa na maelewano mazuri ndani ya
kundi hilo na kuongeza kwa kusema Nahreel
ni Solo Artist
hivyo yeye na Nahreel
hawajavunja kundi hilo na si kwamba mapenzi yake yeye na Nahreel ndiyo sababu
iliyopelekea kuvunjika kwa kundi hilo.
Nahreel na Aika wanatarajia kuachia
ngoma yao ya kwanza wakiwa kama Solo
Artists tarehe 14 mwezi huu.
HABARI MUHIMU: WIFI ANG'ATWA ULIMI MPAKA KUKATIKA
MWALIMU wa Shule ya Msingi Mfaranyaki iliyopo Manispaa ya Songea, Theresia Fuli anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumjeruhi kwa kumng’ata ulimi hadi kukatika wifi yake kwa wivu wa mapenzi.
Akizungumza kwa tabu na gazeti hili jana kwenye
hospitali ya mkoa alikolazwa wodi daraja la kwanza kwa ajili ya
matibabu, majeruhi huyo Oliga Msigale mkazi wa Msamala amesema, bado ana
maumivu makali ya ulimi ingawa amepatiwa matibabu.
Amesema siku ya tukio alishangaa kuona anavamiwa
na wifi yake ambaye ni mtalaka wa kaka yake, ambapo alimtupia mtoto
mkubwa wa kaka yake maharage ya moto kisha kumvamia yeye, huku
akimtuhumu kuwa ndiye binti ambaye amechukua nafasi yake bila kujua kuwa
yeye ni ndugu wa mume na alipoanguka chini alikabwa koo na alipotoa
ulimi nje mwanamke huyo bila huruma alimngata ulimi na kutoa kipande cha
ulimi kisha akatoroka eneo hilo.
Tuesday, 12 February 2013
HABARI MUHIMU: POLISI KUWASAKA WOTE WANAOMTUKANA ANNE MAKINDA
POLISI mkoani Dar es Salaam wametangaza kuwafuatilia, kuwasaka na kuwachukulia hatua wote waliotuma ujumbe wa matusi ama kupiga simu ya vitisho kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda.
Viongozi wa Chadema walifanya mkutano wao
mwishoni mwa wiki kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, jijini Dar es
Salaam na kutoa namba za Spika wa Bunge ili mashabiki wamshinikize
ajiuzulu.
Pia viongozi hao walitoa namba za simu za Naibu Spika, Job Ndugai ili naye ashinikizwe ang’oke katika nafasi yake kwa madai ya kukandamiza upinzani bungeni.
Pia viongozi hao walitoa namba za simu za Naibu Spika, Job Ndugai ili naye ashinikizwe ang’oke katika nafasi yake kwa madai ya kukandamiza upinzani bungeni.
Chadema walidai kuwa Makinda na Ndugai
HABARI MUHIMU: MKUU WA MAJESHI GUINEA AFARIKI KATIKA AJALI YA NDEGE
Mkuu wa jeshi la Guinea, ameuawa kwenye ajali ya ndege katika nchi jirani ya Liberia, akiwa na maafisa wegine watano.
Waliarifiwa kuwa hapakuwa na manusura wa ajali hiyo lakini haikufahamika mara moja idadi ya watu waliokuwa kwenye ndege hiyo.
Baadhi walisema kuwa ni wanajeshi 18 waliokuwa wameabiri ndege hiyo.
Kwa mujibu wa waziri wa habari ,ndege yenyewe ilianguka mjini Charlesville, karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Liberia.
Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirlief, alizuru eneo la ajali, Kusini mwa Monrovia.
Kulingana na shirika la habari la AP, kifo cha Jenerali Diallo, kilitangazwa na rais wa Guinea.
Rais alielezea kusikitishwa na habari za kifo hicho, alipokuwa anakitangaza.
Subscribe to:
Posts (Atom)





