Uhuru Kenyatta ndiye Rais wa nne wa Jamuhuri ya Kenya baada ya tume ya
uchaguzi kumtangaza kushinda uchaguzi wa kihistoria wa Kenya.
Ni baada ya siku tano tangu wakenya kupiga kura kumpigia kura rais,
magavana, maseneta , waakilishi wa bunge, waakislihi wanawake na waakilishi
wodi.
Uhuru alipata zaidi ya asilimia hamsini ya kura zilizohitajika ili
kuapata ushindi kulingana na mahitaji ya katiba mpya ya nchi.
Matokeo hayo yalionyesha kuwa Uhuru Kenyatta ameshinda na kuepuka duru
ya pili ya uchaguzi.
Takwimu kutoka tume ya uchaguzi zinasema Kenyatta ameshinda asilimia
hamsini nukta tatu za kura zote zilizopigwa.
Tume ya uchaguzi ilichukua zaidi ya masaa matano kukagua hesabu ya kura
hizo kabla ya kutangaza matokeo hii leo siku tano baada yawakenya kupiga kura.
Matokeo yaliyotolewa na tume ya uchaguzi yanaonyesha kuwa Uhuru alipata
kura 6,173,433 huku mpinzani wake Raila Odinga akipata 5,340,546
Uhuru Kenyatta
Kenyatta anakabiliwa na mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya ICC
kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007.
Awali duru zilisema iwapo Kenyatta atakabidhiwa ushindi katika raundi
ya kwanza, mpinzani wake waziri Mkuu Raila Odinga atakwenda mahakamani kupinga
matokeo hayo.
Tume hiyo pia itatangaza mshindi wa uchaguzi huo na vile vile kama
mshindi huyo ametimiza masharti ya kikatiba ya kutangazwa kuwa rais wa nne wa
Kenya.
Kamishna Yusuf Nzibo alitoa taarifa hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa
Tume Isaack Hassan.
Vile vile mgombea huyo pia lazima awe ameshinda asilimia 25% katika
nusu ya County zote 47 nchini kenya.
Awali Waziri Mkuu Raila Odinga alikuwa amewaalika waandishi wa habari
nyumbani kwake kwa mkutano maalum ili azungumzie maswala ya matokeo ya urais
lakini baadaye mkutano huo uliakhirishwa hadi siku ya Jumamosi , baada ya tume
ya uchaguzi kutoa tangazo lake la mwisho.
No comments:
Post a Comment