Kundi ambalo
lilikuwa linaundwa wasanii wanne kwa pamoja likiitwa Pah One sasa limevunjika
kwani First Lady
wa kundi hilo la Pah One
mwanadada Aika
ametangaza kujitoa rasmi kwenye kundi hilo pamoja na rapper na producer wa
kundi hilo Nahreel
na hivyo kundi hilo kubakiwa na wasanii wawili tu.
Aika amesema kuwa sababu ya
kumfanya ajitoe kwenye kundi hilo ni kutokuwa na maelewano mazuri ndani ya
kundi hilo na kuongeza kwa kusema Nahreel
ni Solo Artist
hivyo yeye na Nahreel
hawajavunja kundi hilo na si kwamba mapenzi yake yeye na Nahreel ndiyo sababu
iliyopelekea kuvunjika kwa kundi hilo.
Nahreel na Aika wanatarajia kuachia
ngoma yao ya kwanza wakiwa kama Solo
Artists tarehe 14 mwezi huu.
Huko Ujerumani, msemaji wa
serikali amesema kuwa anaheshimu kazi kubwa iliyofanywa na Papa huyu
aliyezaliwa katika Jimbo la Bavaria la nchini humo.
Askofu mkuu wa Canterbury amesema amazipokea taarifa za kujiuzulu kwa Papa kwa huzuni mkubwa ingawa anaelewa undani wa hatua yake.
Kiongozi wa Ujeremani, Bi. Angela Merkel amesifu mchango wa Papa wa kupendekeza mjadala baina ya makanisa, waislamu na wayahudi.
Alikumbusha hotuba ya Papa alipozuru bunge la Ujerumani mnamo mwaka 2011.








