Language

Tuesday, 19 February 2013

RIPOTI MAALUMU YA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012-2013

MATOKEO ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana yametangazwa. Watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6 wamepata sifuri, huku wanafunzi 23,520 tu ambao ni sawa na asilimia 5.16 ndiyo waliofaulu na wengine 103,327 sawa na asilimia 26.02 wamepata daraja la nne.
Akitangaza matokeo hayo jana, Waziri wa Elimu Dk Shukuru Kawambwa alisema watahiniwa walikuwa 456,137, wa shule wakiwa 397,136 huku wa kujitegemea wakiwa 68,806.
“Matokeo ya mwaka huu yamekuwa mabaya sana, Serikali tunasikitika kutokana na hali hii lakini tuna mipango mbalimbali ya kuhakikisha tunaweza kutatua hili tatizo,” alisema Dk Kawambwa.
Dk Kawambwa alisema watahiniwa wote kwa ujumla waliosajiliwa walikuwa 480,036 kati yao wasichana 217,583 sawa na asilimia 45.33 na wavulana 262,453 sawa na asilimia 54.67 lakini waliofanya mtihani huo ni 456,137 sawa na

Wednesday, 13 February 2013

MICHEZO: HILI NDILO BASI LILILOTOLEWA NA TBL MAALUMU KWA TIMU YA TAIFA STARS



HABARI MUHIMU: AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA MBEYA

Mahakama kuu kanda ya Mbeya imemhukumu PETER MWAFRIKA mkazi wa Ndolezi wilayani Mbozi kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia.



Akisoma hukumu hiyo iliyochukua saa 1.30 Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya mbeya NOEL CHOCHA amesema licha ya mikono ya mahakama kufungwa kutoa adhabu ndogo kwa kosa la maauaji ya kukusudia, pia adhabu hiyo ni hatua ya kukomesha watu wenye tabia kama za mtuhumiwa kujichukulia hatua mikononi mwao.
Akirejea mazingira ya kesi hiyo jaji Chocha amesema mnamo Februaly 11,2010 Mshatakiwa na wenzake watatu walifanya kosa la mauaji ya kukudia chini ya kifungu 196 chasheria ya

mwenendo wa makosa ya jinai kwa kumuua KOSAM MWAFRIKA ambaye ni kaka wa marehemu katika kijiji cha Shaji kwa kumkata koromeo na kulitenganisha vipande viwili.
Jaji Chocha katika maelezo yake alisema mshtakiwa akiwa na wenzake ambao walitoweka baada ya mauaji hayo walimvamia Kosam akiwa na mkewe shambani

MICHEZO: MATOKEO NA RATIBA YA MECHI KUBWA ZA LEO DUNIANI


HABARI PICHA: MGAWANYIKO UNASHIKA KASI TANZANIA, HIZI NDIO BUTCHER ZA WAKRISTO


HABARI MUHIMU TOKA GPL: FREEMASONS WAUTEKA MJI WA MOSHI

IMANI ya jamii ya siri ya Freemasons imeonekana kuuteka Mji wa Moshi na vitongoji vyake kutokana na matangazo mengi kubandikwa kila kona yakihamasisha wafuasi kujiunga huku ofa ya utajiri ikipewa kipaumbele.

Risasi Mchanganyiko limeshuhudia matangazo mengi yanayohamasisha kujiunga na imani hiyo yakiwa yamebandikwa kila kona ya mji huu ikiwemo katika nguzo za umeme
Katika tangazo hilo, wahusika wameeleza kwamba watakaojiunga mapema watapewa magari ya kifahari na nyumba za kisasa ikiwa ndiyo njia za awali za kubadilisha maisha yao.
Mwandishi wetu alijifanya anataka kujiunga na kupiga namba za simu zilizowekwa katika tangazo hilo ambazo ni 0783 127 967 ambapo ilipokelewa na mwanaume aliyekataa kutaja jina lake lakini alitoa masharti ya kujiunga.
“Tuma majina yako matatu; lako, baba na babu yako halafu tuma na shilingi 100,000 kwenye namba 0714 084 841 ambayo ni ada ya uanachama kisha utakwenda Kindoroko Hotel, chumba namba 87 hapo utakutana na bosi wangu na utaandikishwa rasmi na kupewa nguo zenye nembo yetu,” alisema mtu huyo.

Mwandishi wetu alifika katika Hoteli ya Kindoroko iliyopo mjini hapa juzi, Jumapili Februari 10, mwaka huu, akaonana na mtu wa mapokezi na kujitambulisha kama mwanachama mpya anayetaka kuonana na mhusika aliyepanga chumba namba 87.
Cha kushangaza, mhudumu alimwambia hawana mteja wa aina hiyo katika hoteli yao na kwamba hakuna chumba chenye namba aliyoelekezwa, jambo lililoonesha wazi kuwa wahusika ni matapeli wanaotaka kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu.
Naye meneja wa hoteli hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Sara alipopigiwa simu, alitoa majibu kama ya mtu wa mapokezi.
Upekuzi wa gazeti hili umebaini kuwa, simu namba 0714 084841 iliyotakiwa kutumiwa fedha na mtu aliyejiita wa Freemasons imesajiliwa kwa jina la Flora Tuvana.
 

TAARIFA YA KIFO CHA MSANII WA TMK WANAUME HALISI 'BK'


HABARI MUHIMU-OLE WAO WANAWAKE WAVUTAJI WA SIGARA

Wataalamu wa afya wanasema kuwa wanawake barani Ulaya wanafariki zaidi kutokana na saratani ya mapafu kuliko saratani ya matiti.

 

Wanaelezea kuwa saratani ya mapafu ndio imekuwa sasa saratani nambari moja ambayo inasababisha vifo miongoni mwa wanawake.
Hali hii tayari inashuhidiwa nchini Uingereza na Poland.
Kulingana na watafiti, hii ni ishara ya idadi kubwa ya wanawake wanaovuta sigara hali iliyoanza kujitokeza kuanzia mapema miaka ya tisini na sabaini.
Idadi ya vifo vinavyotokana na saratani ya mapafu, vitaendelea kuongezeka katika miaka ijayo, lakini sasa kwa sababu ya vijana wa kike wasiovutiwa na kuvuta sigara na ambao idadi yao sio kubwa sana , huenda vifo hivyo vikapungua.
Mwaka 2013, takriban wanawake 82,640 barani Ulaya watafariki kutokana na saratani ya mapafu ikilinganishwa na wanawake 88,886 watakaofariki kutokana na saratani ya matiti.
Wanatarajiwa kuwa vifo vinvyotokana na saratani ya mapafu kupungua mwaka 2020 au 2025 kwa sababu angalu vijana wa kiike hawavuti sana sigara.
Lakini ifikapo mwaka 2015, wanawake wengi watafariki kutokana na saratani ya mapafu kuliko saratani ya matiti, kulingana na mtaalamu wa afya ya wanawake, Profesa Carlo La Vecchia .
Takwimu zinaonyesha kuwa ingawa watu wengi zaidi wanaugua saratani, kwa sababu wanaishi muda mrefu zaidi,
ni watu wachache sana wanafariki kutokana na saratani.

Licha ya kupungua kwa idadi ya watu wanaofariki kutokana na saratani barani humo, idadi ya wanawakewanaofariki kutokana na saratani ya mapafu inaongezeka katika nchi zote za Ulaya.
Profesa La Vecchia,wa chuo kikuu cha Milan, Italy, anasema kuwa hali hii inaleta wasiwasi kwa sababu hakuna dalili kuwa ugonjwa huo unapungua.
Uvutaji sigara pamoja na ugonjwa wa sukari ndio vinachangia kuongezeka kwa ugonjwa huu. Lakini wataalamu wanasema bado hawajui nini kinasababisha sehemu kubwa ya saratani hiyo.
Wataalamu wanasema kuna umuhimu wa wanawake kuwacha kuvuta sigara

BURUDANI: N'SYNC-THIS I PROMISE LYRICS

"This I Promise You"
Ohh ohh...

When the visions around you,
Bring tears to your eyes
And all that surround you,
Are secrets and lies
I'll be your strength,
I'll give you hope,

BURUDANI: TID NAYE KWENDA BIG BROTHER AFRICA



Baada ya jana kusikia kuwa q chifu kachukua form TID nayeye naye kachukua form ya kushiriki big brother  na kufiksha idadi ya wasanii wa ongo kuwekahistoria ya kuchukua form za big brother ambako wema sepetu na nyeye aliichukua q cheaf na hemed pia wato kwenye nia ya kubeba kitita cha dola za kimarekani 300,000
Mshiriki wa mwaka jana Julio aliongea nakusema mtu kama TID angefaa sana kushiriki shindano hilo maana ni mcheshi na ana vigezo vingi vitavyomuwezesha kushinda.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...