Language

Monday, 25 February 2013

MICHEZO: MATOKEO YOTE YA MECHI KUBWA ZA JANA YAKO HAPA


MICHEZO:NIYONZIMA"TUTALIPA KISASI KWA KAGERA SUGAR

KIUNGO wa Yanga, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima, amesema kwamba watalipa kisasi cha kufungwa 1-0 na Kagera Sugar wakati watakaporudiana na timu hiyo kesho, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana, Niyonzima alisema kwamba wamepania kushinda mechi zote zilizobaki za Ligi Kuu ili kuchukua ubingwa kwa heshima kubwa.
Amesema kwanza lazima walipe kisasi cha kufungwa na Kagera katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu, mwaka jana Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
“Kagera walitufunga Bukoba, na sisi lazima tuwafunge hapa Jumatano. Lakini kikubwa ni kampeni yetu ya kushinda kila mechi ili tuchukue ubingwa kwa heshima kubwa,”alisema.
Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Rwanda, alisema

HABARI PICHA: HII NDIO NYUMBA YA DIAMOND PLATNUMZ INAYOTARAJIWA KUGHARIMU KIASI CHA MILIONI 260 MPAKA KUKAMILIKA



HABARI MUHIMU: ANALOJIA KUZIMWA MWANZA FEBRUARI 28

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema inatarajia kuzima matangazo ya mfumo wa analojia mkoani hapa Februari 28, mwaka huu, hivyo kuwataka wananchi kuchangamkia fursa ya kujiunga na mfumo mpya wa utangazaji wa dijitali.


Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA, Habbi Gunze, alibainisha hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari mjini hapa.


Alisema matangazo rasmi ya mfumo wa dijitali mkoani hapa Machi mosi mwaka huu, na kwamba TCRA ipo kwenye mchakamchaka wa kutekeleza mipango yake ya makubaliano na nchi nyingine za Afrika Mashariki katika suala zima la kujiunga na mfumo wa dijitali.

VICHWA VYA HABARI VILIVYOBEBWA NA GAZETI LA CHAMPION


HABARI MUHIMU: PADRI WA UINGEREZA ALIYEJIUZULU KISA KASHFA YA NGONO HUYU HAPA

Mmoja wa mapadre waandamizi wa kanisa katoliki nchini Uingereza amejiuzulu wadhifa wake kufuatia shutma za kwamba alikwenda kinyume na matakwa ya kipadre mapema miaka ya themanini.
Kardinal Keith O'Brien ameachia madaraka kama kiongozi mkuu wa kanisa katoliki nchini Scotland na hatarajii kusafiri kwenda Vatican baadaye mwaka huu kumchagua Papa ajaye baada ya baba Mtakatifu Benedict wa 16 kijuzuru.
Inaarifiwa Padre O'Brien aliwauvinjia heshima makasisi mingo mitatu iliyopita.

HABARI MUHIMU: HUU NDIO MTANDAO WA UJAMBAZI MBEYA DAR ES SALAAM, IRINGA NA MOROGORO

POLISI mkoani Mbeya kwa kushirikiana na polisi mkoani Iringa wamegundua mtandao wa majambazi Sugu ambao umekuwa ukihusika na matukio ya mauaji na unyang’aji wa kutumia silaha. 


 Kamanda wa polisi mkoani hapa Diwan Athumani amesem leo(Feb 25) kuwa watu 13 wakiwemo askari wawili wanashikiliwa huku wengine 16 wakiendelea kufanyiwa uchunguzi na jeshi hilo. Kamanda Athumani aliwataja askari waliokamatwa kuhusika na mtandao huo kuwa ni MT 85393 Samwel Balumwina(31) wa kikosi cha 844 KJ cha Jeshi la kujenga Taifa(JKT) Mbeya na polisi G 9101 PC Samwel Kigunye(27) wa kikosi cha kutuliza ghasia(FFU) Mbeya. Alisema askari hao wamekuwa wakihusika na mtandao wa ujambazi kwa kuazimisha sare za polisi na jeshi la wananchi(JWTZ) kwa wenzao wanaokwenda katika matukio ya uvamizi na kusisitiza kuwa

Tuesday, 19 February 2013

MICHEZO: MECHI MBALI MBALI ZA LEO


RIPOTI MAALUMU YA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012-2013

MATOKEO ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana yametangazwa. Watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6 wamepata sifuri, huku wanafunzi 23,520 tu ambao ni sawa na asilimia 5.16 ndiyo waliofaulu na wengine 103,327 sawa na asilimia 26.02 wamepata daraja la nne.
Akitangaza matokeo hayo jana, Waziri wa Elimu Dk Shukuru Kawambwa alisema watahiniwa walikuwa 456,137, wa shule wakiwa 397,136 huku wa kujitegemea wakiwa 68,806.
“Matokeo ya mwaka huu yamekuwa mabaya sana, Serikali tunasikitika kutokana na hali hii lakini tuna mipango mbalimbali ya kuhakikisha tunaweza kutatua hili tatizo,” alisema Dk Kawambwa.
Dk Kawambwa alisema watahiniwa wote kwa ujumla waliosajiliwa walikuwa 480,036 kati yao wasichana 217,583 sawa na asilimia 45.33 na wavulana 262,453 sawa na asilimia 54.67 lakini waliofanya mtihani huo ni 456,137 sawa na
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...