Language

Friday, 18 January 2013

MICHEZO: CAPE VEDGE KUFUZU KWA RAUNDI YA PILI ?

Mlinda lango wa Cape Verde, Guy Ramos amesema ana matumaini makubwa kuwa taifa lake ambalo linashiriki katika fainali hizo kwa mara ya kwanza litafuzu kwa raundi ya pili kwa fainali.

Cape Verde inachuana na wenyeji wa mashindano hayo Afrika Kusini katika mechi ya ufunguzi siku ya Jumamosi.
Ramos amesema ''ikiwa tutacheza mechi hiyo vyema bila shaka watafuzu kwa raundi ijayo''.
Ramos, ambaye anaichezea klabu ya RKC Waalwijk, ya Uholansi, alisema ''kama timu ya nchi ndogo zaidi barani Afrika, hakuna anayetarajia kuwa watashinda mechi yoyote, lakini tulishinda Cameroon 4-0, ambayo ni nchi kubwa na kinyume na matarajio ya wengi tulishinda. Kwa hivyo mbona sisi tusiwashinde Bafana Bafana?''

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...