Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amelazwa tena hospitalini
baada ya kuugua ugonjwa wa mapafu kwa mara nyingine.
Taarifa kutoka kwa serikali ya nchi hiyo, ilisema kuwa Mandela mwenye
umri wa miaka 94 alilazwa hospitalini muda mfupi kabla ya saa sita usiku.
Mandela alilazwa siku kumi na nane hospitalini mwezi Disemba mwaka jana
kupokea matibabu ya ugonjwa wa mapafu na kibofu.
Anasifika sana kama baba wa taifa hilo kwa kuongoza vita dhidi ya
utawala wa ubaguzi wa rangi.
Kadhalika Mandela alihudumu kama rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini
tangu mwaka 1994 hadi mwaka 1999, ingawa hali yake ya kiafya imezua wasiwasi
kwa muda sasa.
Rais Jacob Zuma alimtumia taarifa ya kumpa pole na kumtakia kupona
Mandela
"tunawataka watu wa Afrika Kusini pamoja na duniani kote kuwa
watulivu na kumuombea Madiba na familia yake. Tuna imani kuwa kikosi cha
madaktari wanaomtibu Mandela watafanya kila hali kuhakikisha anapona,'' alisema
Zuma katika taarifa yake.
Mapema mwezi huu bwana Mandela alilazwa hospitalini mjini Pretoria
baada ya kufanyiwa ukaguzi wa kiafya.
No comments:
Post a Comment