FLAVIANA Matata, mwanamitindo wa kimataifa kutoka Tanzania,
ameshinda tuzo ya ‘Nigeria’s Next Super model 2012’ inayomtambulisha
kama Mwanamitindo Bora mwenye Mvuto Afrika (Africa’s Most Outstanding
Model 2012).
Ushindi wa tuzo hiyo ya pekee kwa aina yake,
umefungua milango ya kutambulika zaidi Matata hata kulivusha kimataifa
jina la Tanzania katika tasnia ya mitindo na mavazi.
Akiongelea ushindi wa tuzo hiyo, Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Compass Communication Tanzania Limited, Maria
Sarungi Tsehai alisema ushindi wa Matata ni mafanikio mengine ya
kujivunia. Tsehai ndiye aliyevumbua kipaji cha Matata.
Kwa mara ya kwanza Flaviana aliibuka kwenye
mashindano ya Miss Universe akiweka rekodi ya mrembo wa kwanza kushinda
taji hilo nchini.
Aliiwakilisha nchi kwenye mashindano ya ‘World Miss Universe’ mwaka 2007 na kumaliza nafasi ya sita, mjini Mexico City, Mexico.
Matata pia ni balozi wa taasisi ya kusaidia watoto
(SOS) na Matata Diamond Empowerment Fund (Def) ya Marekani, ambapo
anafanya kazi sambamba na mwanamitindo na msanii wa vipindi vya
televisheni Kim Kardashian.
Kimwana huyo pia ana mkataba na kampuni ya mitindo
ya Afrika Kusini inayojulikana kama Boss Models SA, ambapo awali pia
aliwahi kufanya kazi na