WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe amekutana na malalamiko
mazito kutoka kwa Chama cha Wakala wa Forodha (TAFFA) ambao wamedai kuna
wamiliki wa meli ambao pia wanafanya kazi ya kuingiza na kutoa mizigo bandarini
jambo ambalo ni kinyume cha sheria.Kwa mujibu wa sheria za Mamlaka ya Udhibiti wa Vyombo vya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) ni marufuku kampuni ya wakala wa meli kuwa na leseni ya kuingiza na kupakuwa mizigo bandarini.





