Vichwa Vya Habari
Language
Friday, 18 January 2013
MICHEZO: CAPE VEDGE KUFUZU KWA RAUNDI YA PILI ?
Mlinda lango wa Cape Verde, Guy Ramos amesema ana
matumaini makubwa kuwa taifa lake ambalo linashiriki katika fainali hizo
kwa mara ya kwanza litafuzu kwa raundi ya pili kwa fainali.
Ramos amesema ''ikiwa tutacheza mechi hiyo vyema bila shaka watafuzu kwa raundi ijayo''.
Ramos, ambaye anaichezea klabu ya RKC Waalwijk, ya Uholansi, alisema ''kama timu ya nchi ndogo zaidi barani Afrika, hakuna anayetarajia kuwa watashinda mechi yoyote, lakini tulishinda Cameroon 4-0, ambayo ni nchi kubwa na kinyume na matarajio ya wengi tulishinda. Kwa hivyo mbona sisi tusiwashinde Bafana Bafana?''
Thursday, 17 January 2013
HABARI: TIGO IMEGOMA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UPIGAJI SIMU
Naibu Mkurugenzi wa Utekelezaji wa Kanda wa TCRA, Victor Nkya, alisema punguzo hilo ni la kutoka asilimia 35 hadi asilimia 69 na kwamba litaanza kutumika Machi mosi mwaka huu
.WAKATI Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwasilisha rai ya kupunguza gharama za mwingiliano wa simu , Kampuni ya Tigo imekataa kufanya hivyo kwa madai kuwa itahatarisha uwekezaji wake kwa punguzo la asilimia 69.
.WAKATI Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwasilisha rai ya kupunguza gharama za mwingiliano wa simu , Kampuni ya Tigo imekataa kufanya hivyo kwa madai kuwa itahatarisha uwekezaji wake kwa punguzo la asilimia 69.
Msimamo huo wa Tigo, umekuja baada ya TCRA kukutana na wadau wa mawasiliano jana jijini Dar es salaam, ili kukusanya maoni kuhusu mapendekezo ya kupunguza gharama ya mtandao mmoja kwenda mwingine. Hatua hiyo inalenga katika kuwasaidia wananchi kumudu gharama za mawasiliano ya simu.
Naibu Mkurugenzi wa Utekelezaji wa Kanda wa TCRA, Victor Nkya, alisema punguzo hilo ni la kutoka asilimia 35 hadi asilimia 69 na kwamba litaanza kutumika Machi mosi mwaka huu na kukoma Desemba 31 mwaka 2017 .
Nkya alisema punguzo la gharama ya kupiga mtandao mmoja kwenda mwingine kwa mwaka 2013 litakuwa asilimia 34.92, mwaka 2014 asilimia 32.40, mwaka 2015 asilimia 30.18, mwaka 2016 asilimia 28.57 na mwaka 2017 ni asilimia 26.96.
“Lengo letu ni kupunguza gharama za mwingiliano wa simu, mfano mwananchi ambaye yupo Tigo anapiga kwenye mtandao wa Vodacom hizi gharama atazilipa mwenye kampuni ya Vodacom kuilipa kampuni ya Tigo badala ya kulipa mwananchi kama ilivyo sasa,” alisema.
Alisema maoni yanayotolewa na wadau yatachukuliwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mawasiliano na kuyafanyia kazi.
Alisema maoni yanayotolewa na wadau yatachukuliwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mawasiliano na kuyafanyia kazi.
Ofisa Mdhibiti wa Kampuni ya Tigo, Levocatus Nkata, alisema punguzo hilo ni kubwa hivyo wawekezaji watashindwa kuendesha kampuni zao.
Alisema Kampuni ya Tigo inatoa huduma zake hadi vijijini na kwamba hatua hiyo itaifanya ishindwe kupeleka na kutoa huduma kwenye maeneo hayo.
Alisema Kampuni ya Tigo inatoa huduma zake hadi vijijini na kwamba hatua hiyo itaifanya ishindwe kupeleka na kutoa huduma kwenye maeneo hayo.
Nkata alisema itachukua muda mrefu kurudisha gharama walizotumia kuendeshea kampuni yao kutokana bei ya kuendesha mitambo.
“Sisi hatukubaliani na hayo mapendekezo yaliyoletwa na TCRA, punguzo hilo kwa sisi wawekezaji ni kubwa sana, tunachoomba wasipunguze ibaki kama ilivyo na kwa mwaka 2017 tunaomba ipunguze kufikia asilimia 45 tu, “alisema Nkata.
Kampuni za Airtel, Vodacom , Benson na Dovetel zimekubali punguzo hilo lakini zimeiomba TCRA ipunguze asilimia chache.
MICHEZO: SUAREZ AKIRI KUJIANGUSHA KATIKA MEHI DHIDI YA STOKE CITY
Msambulizi wa liverpool, Luis Suarez, ana amini kuwa analengwa sana na vyombo vya habari vya Uingereza lakini amekiri alijiangusha katika mechi moja ya ligi kuu msimu huu.
Suarez ambaye ndiye mfungaji bora wa liverpool msimu huu huku akiwa amefunga magoli 15, mawili nyuma ya nyota wa manchester United Robin van Persie, amekiri alijiangusha wakati wa mechi yao na Stoke City tarehe saba October mwaka uliopita.
Tangazo hilo la suarez limemuudhi kocha wa liverpool brendan roggers, ambaye amesema, mchezaji huyo ataadhibiw kuambatana na sheria za klabu hiyo.
Roggers, ametaja tangazo hilo la Suarez, kama moja ambalo kamwe halikubaliki.
MICHEZO: PEP GUARDIOLA AMWAGA WINO BAYERN MUNICH MIAKA 3
Pep Guardiola, mwenye
umri wa miaka 41, awali ilidhaniwa angelijiunga na Chelsea, au Manchester City,
zote za Uingereza.
Guardiola ametia saini
mkataba wa miaka mitatu na Bayern Munich, hadi mwaka 2016.
Atachukua madaraka ya Jupp
Heynckes, ambaye ameamua kustaafu.
Siku zake akiwa mchezaji,
Guardiola, aliwahi kuvichezea vilabu vya Barcelona, Brescia, Roma, Al.-Ahli,
Dorados na pia timu ya taifa ya Uhispania.
Alikabidhiwa pia tuzo nyingi
akiwa mchezaji.
Katika kazi ya meneja,
amewahi kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Uhispania, La Liga, mara tatu, ushindi
wa Supercopa de Espana mara tatu, mara mbili kutwaa ubingwa wa Copa Del Rey,
ubingwa mara mbili wa klabu bingwa barani Ulaya, mara mbili Kombe la Uefa na
vile vile mara mbili ubingwa wa Kombe la Dunia la FIFA kwa upande wa vilabu.
Guardiola, ambaye alizaliwa
tarehe 18 Januari, mwaka 1971, Santpedor, Uhispania, tangu kuondoka uwanja wa
Nou Camp mwezi Mei mwaka 2012, amepumzika msimu mzima, baada ya kukiwezesha
klabu kupata jumla ya vikombe 14, ikiwa ni pamoja na ushindi wa klabu bingwa
barani Ulaya mara mbili.
HABARI: WANAJESHI 200 WA NIGERIA KWENDA KUONGEZA NGUVU MALI
Takriban wanajeshi 200 wa Nigeria wanatarajiwa
kuwasili nchini Mali kusaidia katika harakati dhidi ya wapiganaji wa
kiisilamu Kaskazini mwa nchi.
Jumla ya wanajeshi 3,300 wa kikanda
watapelekwa nchini Mali chini ya azimio la Baraza la Usalama la umoja wa
Mataifa. Chad imesema itapeleka wanajeshi 2,000.
Duru zinasema kuwa makabiliano yalizuka kati ya waasi na wanajeshi mjini Diabaly, umbali wa kilomita 350 kaskazini mwa mji mkuu Bamako siku ya Jumatano.
Wednesday, 16 January 2013
MICHEZO: EMMANUEL OKWI AIAGA RASMI SIMBA SC
SHAMBULIAJI wa Simba SC, Mganda
Emmanuel Okwi ameuzwa klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia kwa dola za
Kimarekani 300,000.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema mida hii kwamba,
Okwi amekamilisha vipimo na kila kitu na tayari amesaini mkataba.
“Tunasubiri
kulipwa fedha zetu tu, viongozi watakwenda Tunisia kuchukua fedha za mauzo ya
mchezaji huyo,”alisema Poppe.
Okwi
amekuwa akipiga chenga kuripoti kambini Simba SC na alikuwa hata hapokei simu
za viongozi wa klabu hiyo kila alipopigiwa.
Kufuatia
hatua hiyo, uongozi ulimuengua kwenye programu ya safari ya Oman na sasa
inabainika ametua Sahel.
Baada ya
kumaliza mkataba wake wa awali, Desemba mwaka jana aliongeza mkataba wa miaka
miwili na Simba SC ambao kabla hajaanza kuutumikia, anahamia Sahel.
HABARI: OLE WAKE ATAKAEICHEZEA SERIKALI
Serikali imesema haitavumilia kwa namna yeyote ile vurugu za
kidini, kikanda na ukabila ambazo baadhi yake zilitaka kulitia doa taifa
mwaka jana.

Pia imesisitiza kwamba haitawavumilia wanasiasa wanaotumia rasilimali za taifa kujitafutia umaarufu kwa gharama za kuligawa taifa.

Pia imesisitiza kwamba haitawavumilia wanasiasa wanaotumia rasilimali za taifa kujitafutia umaarufu kwa gharama za kuligawa taifa.
Akizungumza na mabalozi kwa nyakati tofauti
Ikulu, Dar es Salaam; kwanza katika sherehe ya kuukaribisha Mwaka Mpya
iliyofanyika juzi na alipokuwa akiagana na Balozi wa Uingereza nchini,
Dianne Corner jana, Rais Jakaya Kikwete alisema vurugu zilizotaka
kujitokeza mwaka jana zinatosha.
“Serikali haitavumilia vurugu wala ukabila kwa
namna yoyote ile…. Mwaka 2012 vurugu zenye sura ya kidini zilianza
kujitokeza ila sasa nasema kwamba hatutazivumilia kwa namna yeyote ile,
inatosha,” alisema Rais Kikwete.
Akizungumza katika hafla hiyo, Kiongozi wa
Mabalozi ambaye pia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC),
Juma Mpango alisema jumuiya ya mabalozi imefurahishwa na namna ambavyo
Serikali imekuwa ikishughulikia vurugu za kidini ambazo zilitaka
kujitokeza bila kusababisha madhara kwa wananchi.
“Tumeridhishwa na namna ambavyo Serikali
imekuwa inashughulikia mambo yake vizuri. Tunaomba mwendelee
kushughulikia amani ya nchi hii maana ndiyo mhimili wa nchi za Maziwa
Makuu,” alisema Balozi Mpango.
Kuhusu gesi
Rais Kikwete alizungumzia suala la rasilimali za taifa na kusisitiza kuwa pia hatavumilia kuona wanasiasa wakitumia suala la gesi kujitafutia umaarufu.
Wakati Rais Kikwete akitoa kauli hiyo jana,
habari kutoka Mtwara zilidai kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
George Simbachawene amewekewa magogo barabarani kumzuia asiende kwenye
kijiji kinachozalisha gesi hiyo, huku Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea,
Regina Chonjo akizomewa.
Hata hivyo, polisi walikiri wananchi kuweka
magogo barabarani kwa lengo la kumzuia waziri huyo, lakini ikaeleza kuwa
gari lililozuiwa siyo la Simbachawene.
Akizungumza na Balozi Corner, Rais Kikwete
alikemea tabia ya baadhi ya viongozi wa kisiasa kutumia suala la
rasilimali za taifa, ikiwamo gesi asilia kujitafutia umaarufu wa kisiasa
na kuwapotosha wananchi.
“Ni jambo la hatari na lisilo na tija kwa
wanasiasa kujaribu kuigawa nchi vipandevipande kwa sababu ya kujitafutia
umaarufu kwa kutumia rasilimali za taifa,” alisema Rais Kikwete na
kuongeza:
“Unawezaje kuwa na nchi moja na taifa moja
wakati kila mmoja anadai rasilimali kutoka kwenye eneo moja ibakie na
kunufaisha watu wa eneo hilo tu. Huwezi kuwa na nchi moja na yenye umoja
wakati kuna nchi ya gesi asilia kule Mtwara, kuna nchi ya kahawa kule
Kilimanjaro, kuna nchi ya chai na ndizi kule Bukoba,” alisema Rais
Kikwete na kuongeza:
“Kwa sababu kama gesi asilia inatakiwa kubakia
na kunufaisha watu wa Mtwara tu, basi wenye haki zaidi ya kudai jambo
hili siyo watu wa Mtwara, bali ni watu wa Msimbati ambako ndiko
ilipogunduliwa gesi ambako ni maili 60 kutoka Mtwara, kilomita 200
kutoka Newala.”
Subscribe to:
Posts (Atom)



