Language

Wednesday, 9 January 2013

HABARI: KAKOBE AKANA KULITOROKA KANISA


KIONGOZI wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, jijini Dar, Askofu Mkuu Zacharia Kakobe, amekanusha madai ya kutoweka nchini na kusema ni uvumi na hakuna ukweli wowote.                                              

Askofu Kakobe aliyasema hayo, Januari 6, mwaka huu ndani ya kanisa lake alipokuwa akiwahutubia waumini wake na kusema ameshangazwa na baadhi ya vyombo vya habari vilivyosambaza taarifa  kuwa amelitoroka kanisa hilo, kitu ambacho si cha kweli.
“Kunisingizia habari hizo ni kama wananiongezea maono sababu kweli natarajia kuondoka siku za hivi karibuni lakini sikusema ni lini na nitakwenda wapi,” alisema Kakobe.
Akithibitisha juu ya uwepo wake katika kanisa hilo, kiongozi huyo aliendelea kufanya  maombi na ibada zake kama kawaida huku mamia ya waumini wakisubiri uponyaji na wengine wakitoa ushuhuda juu ya miujiza waliyoipokea.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...