WACHEZAJI Andrei Arshavin, Maroune Chamakh, Squillaci ni wachezaji
wanaotajwa kuuzwa huku Manuel Almunia na kipa mwenzie, Vito Mannone
wakiwa tayari wameshapewa baraka za kuondokan Emirates.
Kwa mujibu wa Daily Mail, Arsenal ina mpango wa kuwapunguza wachezaji
hao mwezi ujao katika kipindi cha dirisha dogo kutokana na kushindwa
kucheza vizuri katika mechi yao ya Ligi ya Mabingwa mjini, Athens
Ugiriki.
Arsenal pia itasikiliza ofa ya kumtaka mchezaji Tomas Rosicky, ingawa
klabu inahofia kutopata viungo mbadala, huku Jack Wilshere akiwa
majeruhi. Arsenal iliwaacha wachezaji watano katika majira ya joyo
yaliyopita. Wilshere atasubiri hadi wiki hii kuona kama atapewa adhabu kutokana na
kuvunja sheria inayokataza wachezaji kucheza kamari ya kutabiri.
Kabla ya mechi ya Jumanne iliyopita dhidi ya Olympiakos, kiungo huyo
alisema kwenye mtandao wake kuwa anatabiri Emmanuel Frimpong kufunga bao
la kwanza.
Wilshere baadaye aliandika tena kwenye mtandao wake na kukanusha
kutabiri. Shirikisho la soka la Ulaya linakataza wachezaji kuhusika
utabiri wa mechi.
No comments:
Post a Comment