Language

Saturday, 19 January 2013

MICHEZO: ARMSTRONG ALILIA KIFUNGO CHAKE CHA KIFO

Mwendeshaji baiskeli Lance Armstrong ameelezea kushangaa kwa kukabidhiwa adhabu ya maisha ya kutoshiriki katika michezo, ilhali wanamichezo wenzake wamekuwa wakipigwa marufuku ya miezi sita tu
 
Katika sehemu ya pili ya mazungumzo yake na Oprah Winfrey, mwanamichezo huyo mwenye umri wa miaka 41 alisema: "Ninastahili kuadhibiwa. Lakini sidhani ninastahili hukumu ya kifo."
"Ningelitamani sana kupata nafasi ya kushindana, lakini hiyo sio sababu ya yale ninayoyafanya."
Kwa usiku wa pili, mazungumzo yake na Winfrey, mwenye umri wa miak 58, yalipeperushwa katika muda ambao watazamaji wengi walipata fursa ya kutizama televisheni, na yalionekana kote duniani kupitia tovuti yake.
Mazungumzo hayo yalikuwa hewani kipitia kituo cha Winfrey cha televisheni nchini Marekani, OWN, yaani Oprah Winfrey Network.
Katika sehemu ya kwanza ya mazungumzo yao, Mmarekani Armstrong hatimaye alikiri kutumia dawa za kuongezea nguvu michezoni zilizopigwa marufuku, baada ya kukanusha kwa muda wa miaka mingi, na huku akiibuka bingwa mara saba wa mashindano ya baiskeli ya Tour de France.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...