Language

Tuesday, 12 March 2013

HABARI MUHIMU: UCHAGUZI WA PAPA KULETA ZENGWE KAMA UCHAGUZI MKUU KENYA?




Mchakato wa kumchagua Papa mpya wa Kanisa Katoliki umepamba moto wakati misa maalumu ya kuandaa uchaguzi huo ikifanyika katika makao makuu ya Kanisa la Mtakatifu Peter wa Basilica lililopo Vatican.

Makardinali 115 wenye umri wa zaidi ya miaka 80 ambao wanatarajiwa kushiriki uchaguzi huo, watafungiwa ndani ya hekalu la Sistine ambako zoezi zima litafanyika.

Papa Benedict wa 16 alijiuzulu mapema mwezi Februari na kuupa ulimwengu mshtuko baada ya kuwa ni Papa wa kwanza kujiuzulu kwa kipindi cha miaka 600 iliyopita.


Katika hotuba yake ya mwisho, Kiongozi wa Chuo Cha Makardinali, Kadinali Angelo Sodano alihimiza umoja ndani ya Kanisa Katoliki na kuwaasa makadinali watakaopiga kura kuweka pembeni tofauti zao kwa manufaa ya kanisa na kwa Papa wa Mpya.

“Kila mmoja wetu hapa anatakiwa kutoa ushirikiano wake kwa mrithi wa Papa Benedict XVI, tudumishe umoja na mshikamano” alisema Kardinali Sodano Hii ni kauli nzito ya mwisho kutolewa na Kardinali wa Vatican kabla ya kuteuliwa kwa Papa mpya.

Hata hivyo Kardinali Sodano hatashiriki uchaguzi huu kwani ana umri wa zaidi ya miaka 80.
Kabla ya uchaguzi, makardinali wote wataapishwa kwa kula kiapo cha kutunza siri ya matukio yote wakati wa uchaguzi huo.

Aidha imeelezwa kuwa zoezi hilo linaweza kudumu kwa siku kadhaa kwani makardinali hao huenda wakapiga kura zaidi ya mara nne hadi pale mrithi wa Papa atakayeliongoza kanisa hilo lenye waumini zaidi ya bilioni moja duniani atakapopatikana. Makardinali hao watatakiwa kuanza mchakato mzima wa zoezi hilo saa 10.30 leo. Baada ya kula kiapo maneno kama “extra omnes” na kila mmoja yatatamkwa.

Katika mchakato huo makardinali wataandika jina la Papa wanayempendekeza katika kipande cha karatasi na kukirusha katika chombo maalumu.

Watabiri wa mambo wanadai kuwa katika mchakato huo huenda ukatokea uwezekano wa Papa mmoja kati ya makardinali 115 kupata kura 77 au robo tatu, na ndiye atayekuwa papa katika uchaguzi wa kwanza.

Hata hivyo makardinali hao wamekuwa na mtazamo tofauti kuhusu Papa mpya watakayemteua.

Kumekuwa na mawazo tofauti iwapo Papa mpya awe anatoka nje ya Jiji la Vatican au chaguo kutoka ndani ya Vatican ili alete mabadiliko kutoka ndani.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...