
Kutokana na wizi huo kukithiri katika baadhi ya benki, wafanyabiashara na wananchi wameanza kujipanga kuondoa fedha zao katika akaunti.

“Wizi kama huo unatokea wakati mtu anaweka namba za siri kwenye ATM kwani kuna
watu huweka kamera ambazo husoma na namba hizo kufanikiwa kuzipata kisha
kufanya wizi ,” alisema Profesa Ndullu.
Alisema kuwa kutokana na wizi kukithiri wamezitaka benki zote kuweka mifuniko
katika eneo la namba za siri ili wezi wanaoweka kamera ili kuzinasa wakati mtu
anatoa fedha washindwe kufanya hivyo.
Profesa Ndullu alisema wanafuatilia mfumo wa utendaji wa benki ili kuondokana
na tatizo hilo ambalo hivi sasa limeibua mijadala na hofu kubwa miongoni mwa
wananchi.
Benki kubwa nchini zimekumbwa na mtikisiko wa wizi wa fedha kwa kadi za ATM,
ambao umeongezeka kwa kasi kiasi cha kufanya wananchi wengi kuhifadhi fedha zao
kwenye mitandao ya makampuni mbalimbali ya simu za mikononi ambayo hata hivyo
ripoti zimekuwa zikieleza kuwa nako usalama wake si wa kiwango cha juu.
Baadhi ya benki ambazo zimekumbwa na matukio hayo zimekuwa zikisita kutoa
taarifa kueleza sababu za kushindwa kuzuia wizi huo na badala yake zimekaa
kimya kuhofia kupoteza wateja.
Kukua kwa teknolojia za kifedha ambako kumerahisisha ufanisi wa matumizi na
utunzaji wa fedha, sasa kunaonekana kugeuka na kuwa balaa kutokana na kuibuka
kwa wizi mkubwa mahala zinakohifadhiwa kwenye akaunti za wateja kwa kutumia
njia ya mtandao.
Taarifa za wizi huo zilianza kurindima mwezi Machi, 2010, ambako kiasi cha
mabilioni ziliibwa kupitia katika mashine za ATM huku kati ya kiasi hicho jumla
ya Sh360 milioni zikihusisha benki moja nchini.
Hata hivyo, mwaka huo watu wanne walikamatwa baada ya kuripotiwa wizi huo
mkubwa. Sambamba na kukamatwa kwa watu hao, pia alikamatwa mfanyabiashara mmoja
aliyekuwa akifanya jaribio la kuiba kimafia Sh221 milioni kutoka benki ya NBC.
Wimbi la wizi huo limeibuka tena katika kipindi cha Oktoba 2012 hadi Februari
2013 na inakadiriwa kuwa jumla ya kiasi cha Sh700 milioni kimeibwa katika benki
mbalimbali kwa nyakati tofauti.
No comments:
Post a Comment