Kutokana na uamuzi huo hakutakuwa tena na pasi za bure kwa ajili ya
kushuhudia mechi zilizo chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa TFF katika
viwanja mbalimbali nchini.
Uamuzi huo umetokana na ukweli kuwa free pass zimekuwa zikipunguza au
kuchukua mgawo wote wa TFF kwenye mechi, na wakati mwingine Shirikisho
hulazimika kutoa fedha za ziada kugharamia pasi hizo.
Pasi zote ambazo imekuwa ikitoa kwa wadau wake hukatwa katika mgawo wa
TFF katika mechi husika. Shirikisho hivi sasa linapata asilimia nne tu ya
mapato katika mechi za Ligi Kuu, ligi ambayo hivi sasa inaendeshwa na Kamati
yake ya Ligi.
No comments:
Post a Comment