Mchezaji nyota wa Gofu wa Marekani Tiger Woods amewika tena baada ya
kunyakuwa ubingwa katika mchezo huo hapo jana, hii ikiwa ni mara ya kwanza
tangu nyota yake ilipoanza kuburuza mkia.

"Nimecheza vizuri, na ushindi huu unatokana na kutia bidii zaidi
katika kazi yangu na kuwa na subira" alisema Woods. Ushindi wa jana
Jumatatu umempatia nyota huyo wa gofu kitita cha euro milioni 1.08 million.
Baada ya Woods kukabiliwa na kashfa ya kimapenzi iliyozua sintofahamu
kati yake na mkewe miaka mitatu iliyopita na hata majeraha ya mguu aliopata
yalimfanya kuvuta mkia katika mchezo huo wa gofu ambao tangu alipoanza kuucheza
mwaka wa 1997 amewaki kupata ushindi kwa mara 77.

Disemba mwaka huo Tiger Woods alitoa taarifa akikubali kuwa alikuwa na
mahusiano nje ya ndoa yake na kutangaza kuwa anapumzika kutoka kwa mchezo huo
wa Gofu. Baadaye alirudi uwanjani mwaka wa 2010, lakini ndoa kati yake na
mwanamitindo wa zamani Elin Nordegren, ilikuwa imeshavunjika.
Wiki iliopita Woods alitangaza kuwa na mahusiano mapya na Lindsey Vonn
Mmarekani ambaye ni mchezaji wa mchezo wa kuteleza kwenye barafu.
No comments:
Post a Comment