Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imeiahirisha kesi
inayomkabili Mkuu wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Wilfred Lwakatare na Joseph Ludovick hadi Aprili 17, mwaka huu.
Wakili Mwandamizi wa Serikali, Tumaini Kweka aliiambia mahakama hiyo iliyokuwa imeketi chini ya Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana kuwa kesi hiyo jana ilifikishwa kwa ajili ya kutajwa.
Alisema hatua hiyo inatokana na ukweli kwamba jalada kuu la kesi lipo katika
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam.
Baada ya maelezo hayo, Hakimu Katemana aliiahirisha kesi hiyo hadi Aprili 17,
mwaka huu.
Lwakatare na Ludovick wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama ya kutoa sumu kwa nia ya kumdhuru Dennis Msacky, kushiriki katika kupanga njama za utekaji nyara, kushiriki katika mkutano wa kupanga kitendo cha ugaidi cha utekaji nyara.

Akisoma hati ya mashtaka hayo, Wakili wa Serikali, Prudence Rweyongeza alidai
kuwa washtakiwa walifanya hivyo Desemba 28, mwaka jana katika eneo la
King’ong’o wilayani Kinondoni. Washtakiwa kwa pamoja walikula njama kwa kutoa
sumu kwa nia ya kumdhuru Msacky ambaye ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la
Mwananchi.
Wakili huyo wa Serikali pia alidai kuwa Desemba 28, 2012 walishirikiana kupanga
njama za utekaji nyara dhidi ya Msacky.
No comments:
Post a Comment