Mahakama ya rufaa nchini Mirsi imeamuru rais wa zamani wa nchi hiyo,
Hosni Mubarak hapaswi kuzuiliwa tena kuhusiana na vifo vya waandamanaji
waliofariki wakati wa mapinduzi yake.
Lakini Mubaraka atasailia kizuizini huku uchunguzi ukifanywa kuhusiana
na kesi ya ulaghai dhidi yake. Hii ni kwa mujibu wa vyombo vya habari vya
serikali Misri
Mahakama ya rufaa mjini Cairo iliamuru hilo ikisema kuwa Mubaraka
amezuiliwa kwa miaka miwili kipindi kinachoruhusiwa cha mshukiwa yeyote
kuzuiliwa kabla ya kesi kusikilizwa na kuamuliwa.
Kesi dhidi ya Mubarak itasikilizwa tena huku akitaka uamuzi wa kufungwa
maisha jela kubatilishwa.
Aidha Mubarak,aliyetawala Misri kwa miongo mitatu aling'olewa mamlakani
katika mapinduzi ya kiraia mwaka 2011.
Amekuwa akizuiliwa tangu Aprili mwaka 2011 baada ya kuhusishwa na vifo
vya mamia ya waandamanaji waliofanya maandamano ya amani wakimtaka aondoke
mamlakani Januari kati ya tarehe 25-31.
Pia anakabiliwa na kesi ya ufisadi.
Mawakili wake walitaka mahakama kumwachilia Mubaraka kwani amezuiliwa
kwa miaka miwili sasa na kulingana na sheria anapaswa kuachiliwa ikiwa kesi
yake haijaamuliwa.
No comments:
Post a Comment