Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta amewashukuru wananchi pamoja na
Mwenyezi Mungu kwa kumwezesha kushinda nafasi hiyo huku akiahidi kuijenga
upya Kenya.
Uhuru amesema ataweka kipaumbele kwenye kutunza rasilimali za nchi na
kuhakikisha zinawanufaisha wananchi wote, pia kuwawezesha wanawake na vijana.
Katika hotuba yake aliyotoa muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi jana, Kenyatta alisema anawashukuru wagombea alioshirikiana nao katika mchakato wote wa uchaguzi na kuwakaribisha kuungana.
“Nawashukuru wagombea wenzangu wote kwa kujitolea kwa moyo kushiriki katika kinyang’anyiro hiki kwa kuwa jambo hilo limezidi kuonyesha demokrasia iliyopo nchini,” alisema.