Wadau wa elimu Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, mkoani Mara,
wameshauri Serikali kufanya ukaguzi wa kina wa vyeti vya taaluma za walimu, ili
kubaini kama wanaovitumia ndiyo wamiliki wake halisi.
Hatua hiyo inatokana na vyeti hivyo kuonyesha ufaulu mzuri kwa
baadhi ya walimu wilayani hapa, lakini hawana uwezo wa kufundisha darasani.
Wakichangia maoni kwenye mkutano wa kujadili maendeleo ya elimu
wilayani hapa uliofanyika juzi, wadau hao walisema hali hiyo inaifanya shule
kuwa na idadi kubwa ya walimu, lakini hawana taaluma ya ualimu.
Walisema kwamba hali hiyo ndicho chanzo cha kushusha kwa taaluma
shule za msingi na sekondari.










