Jeshi la Jamhuri ya Demokrasi ya Congo linasema kuwa limeikomboa miji
miwili ya mashariki mwa nchi ambayo ilikuwa imedhibitiwa na wapiganaji wa M23
kwa miezi kadha.
Msemaji wa jeshi alieleza kuwa wanajeshi wa serikali wameingia katika
miji ya Rutshuru na Kiwanja baada ya M23 kuondoka
Juma hili M23 waligawanyika mapande mawili ambayo yalianza kupigana.
Maelfu ya watu wamekimbilia nchi ya jirani, yaani Uganda, ili kuepuka
mapigano hayo.
Mapambano yalianza punde baada ya viongozi wa Afrika kutia saini
mkataba wa kumaliza vita vya miongo miwili mashariki mwa Congo.
No comments:
Post a Comment