Wasaidizi wa karibu na ndugu wa rais Hugo Chavez wa Venzuela wamekanusha
habari kuwa rais huyo anaweza kuwa amefariki au anakaribia kufa kutokana na
ugonjwa wa saratani, na kusema kuwa bado anapigana kuokoa maisha yake.
Wasaidizi wa karibu na ndugu wa rais Hugo Chavez wa Venzuela wamepinga
habari zilizosambaa kuwa rais huyo anaweza kuwa amefariki au anakaribia kufa
kutokana na ugonjwa wa saratani, na kusema kuwa bado anapigana kuokoa maisha
yake.
Makamu wa rais wa Venezuela Nicolas Maduro alisema siku ya Ijumaa kuwa
Chavez yuko katika hali nzuri, lakini akipigania maisha yake wakati akifanyiwa
tiba ya kutumia kemikali katika hospitali ya kijeshi mjini Caracas. Ilikuwa
mara ya kwanza kwa Maduro kutangaza kuwa rais huyo ameanza kutumia tiba hiyo ya
kemikali kufuatia upasuaji wa nne wa saratani nchini Cuba mwezi Desemba, na
kuamua kuendelea na matibabu nchini kwake. Alisema Chavez na madakatari wake
waliamua kuanza tiba ya kemikali na mionzi, baada ya hali yake kuboreka mwezi
Januari.
No comments:
Post a Comment