Kiongozi mmoja mkuu wa kundi la wapiganaji la al-Qaeda ameuawa nchini
Mali. Taarifa hizi zimethibitishwa na Rais wa Chad, Idriss Deby
Alisema kuwa majeshi ya nchi yalimuua Abdelhamid Abou Zeid, wakati wa
makabiliano yaliyotokea katika eneo moja la vijijini nchini Mali.
Anasemekana kuwa wa pili kwa ngazi ya uongizi
katika kundi hilo ambalo
linapigana na majeshi ya kigeni nchini Mali.
Raia huo wa Algeria anatuhumiwa kwa mauaji ya mateka wawili kutoka nchi
za magharibi Edwin Dyer raia muingereza mwaka 2009 Michel Germaneau raia wa
ufaransa mwaka uliofuata.
Mwandishi wa BBC Thomas Fessy anasema kuwa ikiwa wataweza kuthibitisha
kifo hicho, maswali bila shaka yataibuka kuhusu mateka wa Ufaransa wanaoaminika
kuwa walikuwa mikononi mwa Abou Zeid.
Mwezi Januari, Ufaransa ilituma wanajeshi 3,500, Kaskazini mwa Mali,
kwa lengo la kuwafurusha wanamgambo wa kiisilamu waliokuwa wameteka sehemu ya
jangwa la Sahara.
Chad ni mojawapo ya nchi nyingi za Afrika ambazo zinaunga mkono
harakati za jeshi la Ufaransa nchini Mali.
No comments:
Post a Comment