Language

Monday, 11 February 2013

HABARI MUHIMU: PAPA BENEDICT XVI AJIUZULU

Huko Ujerumani, msemaji wa serikali amesema kuwa anaheshimu kazi kubwa iliyofanywa na Papa huyu aliyezaliwa katika Jimbo la Bavaria la nchini humo.
 
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron, amemsifu Papa kwa jitihada zake za kuimarisha mahusiano baina ya Vatican na Uingereza.
Askofu mkuu wa Canterbury amesema amazipokea taarifa za kujiuzulu kwa Papa kwa huzuni mkubwa ingawa anaelewa undani wa hatua yake.
Kiongozi wa Ujeremani, Bi. Angela Merkel amesifu mchango wa Papa wa kupendekeza mjadala baina ya makanisa, waislamu na wayahudi.
Alikumbusha hotuba ya Papa alipozuru bunge la Ujerumani mnamo mwaka 2011.

BURUDANI: HII NDIO SIRI YA NE-YO KUVAA KOFIA MUDA WOTE, 'KIPARA' MUANGALIE KATIKA PICHA HII


MICHEZO: MATOKEO YA MECHI ZOTE KUBWA ZA JANA YAKO HAPA PAMOJA NA RATIBA YA MECHI ZA LEO



MITINDO: NGUO BOMBA KWA BRAZAZ



Sunday, 10 February 2013

BURUDANI: DOWNLOAD LET ME LOVE TOU(REMIX) YA NE YO

BURUDANI: LYRICS ZA BOYFRIEND YA JUSTIN BIEBER HIZI HAPA

"Boyfriend"
[Verse 1]
If I was your boyfriend, I’d never let you go
I can take you places you ain't never been before
Baby, take a chance or you’ll never ever know
I got money in my hands that I’d

MICHEZO: NIGERIA MABINGWA WAPYA AFRIKA

Nigeria mabingwa wapya Afrika 2013,yailaza Burkina Faso 1-0 katika mchezo wa fainali nchini Afrika Kusini.

Ni shangwe na vigelegele katika miji mbalimbali nchini Nigeria baada ya timu yao ya The Super Eagles, kuibuka mabingwa wapya wa Kombe la Mataifa ya Afrika.
Mbio za kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika zilizoanza tarehe 19 Januari zimehitimishwa, Jumapili, tarehe 10 Februari kwa Nigeria kuibuka bingwa wa fainali za mwaka 2013 barani Afrika.
Bao la mchezaji Sunday Mba alilofunga katika dakika ya 40 ya kipindi cha kwanza cha mchezo mjini Johannesburg, ndilo lililowahakikishia The Super Eagles, Nigeria kuwa mabingwa wapya.
Mchezo huo ulianza kwa kasi, timu zote mbili zikishambuliana kwa zamu. Hata hivyo Nigeria ndiyo walionekana kutawala zaidi mpambano huo na kukosa magoli kadha ambayo yangeipa ushindi mnono Nigeria.
Wachezaji wa Burkina Faso
Vijana hao wa Super Eagles, wamekuwa wakiimarika kila hatua ya mashindano hayo, hasa baada ya kufuzu kutoka katika makundi. Ni katika hatua ya makundi ambapo mabingwa watetezi, Zambia walitolewa na kuachia kombe hilo kufukuziwa na timu nane zilizoingia robo fainali, na hatimaye timu mbili zilizotinga fainali, Nigeria na Burkina Faso.
Emmanuel Emenike aliibuka mfungaji bora wa mashindano hayo na kupata kikombe, huku Moses Victor akiwa mchezaji bora wa mechi kati ya Nigeria na Burkina Faso.
Mechi hiyo ya fainali ilihudhuriwa na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, akiwa mgeni rasmi, akiambatana na rais wa Fifa Sepp Blatter na rais wa CAF, Issa Hayatou.
The Super Eagles pia waliahidiwa zawadi kem kem, zikiwemo fedha taslim kwa kocha na wachezaji, hata kabla ya kutwaa ubingwa.
Hii ni zawadi kubwa kwa kocha wa Super Eagles, Stephen Keshi ambaye mwaka 1994, wakati Nigeria ilipotwaa ubingwa wa Afrika, alikuwa nahodha wa timu hiyo katika fainali zilifanyika nchini Tunisia.
Pia Nigeria ilitwaa ubingwa mwaka 1980, wakati fainali hizo zilipoandaliwa nchini Nigeria.
Super Eagles kama ilivyo kwa timu nyingine barani Afrika, itakuwa ikijiandaa kikamilifu kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia zitakazofanyika nchini Brazil mwaka 2014.

HABARI MUHIMU: MAJESHI YA MALI YAFIKA GAO

Mapigano baina ya wanajeshi wa serikali ya Mali na wapiganaji wa Kiislamu kwa mara ya kwanza yamefika kati-kati ya mji wa Gao, mji mkubwa kabisa kaskazini mwa nchi.

Mwandishi wa BBC alioko huko anasema wanajeshi wa Ufaransa wanatumia mizinga dhidi ya wapiganaji hao walioingia hapo kabla.
Anasema ghasia zilianza karibu na makao makuu ya polisi, lakini mapigano yametapakaa.
Wanajeshi wa Ufaransa na Mali waliukomboa mji huo mwezi uliopita.
Shirika la habari la Ufaransa linaeleza kuwa wapiganaji wa Kiislamu waliovaa nguo nyeusi, huku wamebeba bunduki, waliteka eneo la kati ya mji wa Gao, mji wenye wakaazi wengi kabisa kaskazini mwa Mali.

MICHEZOl: NIGERIA BINGWA WA AFCON 2013


KIBONZO


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...