Shirika moja lisilo la kiserikali la Ubelgiji APOPO limeanza kuwafundisha
panya namna ya kutambua mabomu yaliyofukiwa ardhini. Panya hao ambao ni wakubwa
kuliko panya wa kawaida wanafanyiwa majaribio Morogoro Tanzania .Inaaminika
wanauwezo mkubwa wa kunusa kuliko mbwa. Hii inatokana na kuwa pua zao zipo
karibu na ardhi,hali ambayo inawasaidia katika kazi yao ya utambuzi wa mabomu.
No comments:
Post a Comment