Kocha wa African Lyon, Charles Otieno amesema kwa sasa wanaomba Toto
African, Polisi Morogoro wapoteze michezo yao ili wasalimike na janga la kushuka
daraja.
Kocha huyo alikiri hawana njia mbadala ya kukwepa janga la kushuka
daraja kama si kuomba dua mbaya kwa Toto na Polisi tu kwa sasa.
“Siwezi kusema tumeshuka, bado tunamichezo mitatu mkononi endapo
tutashinda uwezekano ni mkubwa wa kuendelea kubaki, hakuna njia ya kutubakiza
zaidi ya Polisi na Toto kupoteza mechi zao ili sisi tuweze kupata nafasi
kinyume na hapo ni lazima tutashuka tu”alisisitiza kocha huyo.
Lyon imebakiza mechi dhidi ya JKT Ruvu, Mtibwa Sugar pamoja na Mgambo
JKT. (Jessca Nangawe)Text inakuja hapa.
No comments:
Post a Comment