Huduma za umeme katika Mji wa Zanzibar, jana zilikatika kwa zaidi ya nusu
saa baada ya kuzinduliwa kwa mradi mkubwa wa umeme kutoka Tanzania Bara.
Uzinduzi wa mradi huo, ulifanywa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, katika Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.
Sherehe za uzinduzi wa mradi huo, zilihudhuriwa pia na wananchi wa maeneo
mbalimbali ya Zanzibar.
Hata hivyo muda mfupi baada ya shughuli hizo, huduma za umeme katika
Mji wa Zanzibar, zilikatika kuanzia saa 9 mchana na kudumu kwa zaidi ya
nusu saa.
Meneja wa Shirika la Umeme la Zanzibar (Zeco), Mbarouk Hassan, alithibitisha kuwa huduma zilikatika na kwamba tatizo lilikuwa Tanzania Bara.
Meneja wa Shirika la Umeme la Zanzibar (Zeco), Mbarouk Hassan, alithibitisha kuwa huduma zilikatika na kwamba tatizo lilikuwa Tanzania Bara.
“Umeme ulikatika kabisa, lakini tatizo lilianzia Bara, hata hivyo
limemalizika,” alisema Meneja huyo kwa njia ya simu.
Akizindua mradi huo uliogharimu Dola za Marekani 64.4 milioni Dk Shein
aliwataka wananchi kulinda miondumbinu ya umeme kwa kuzingatia kuwa
inatengenezwa kwa gharama kubwa.
Dk Shein ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar, aliita Zeco kufuatilia madeni yake na kuwataka wananchi kulipia ankara za umeme.
Alisema kufanya hivyo kuatoa fursa nzuri kwa wawekezaji kuwekeza visiwani Zanzibar kwa sababu watakuwa na umeme wa uhakika.

Mradi huo unaotekelezwa kwa msaada wa Marekani, umeanzia Ras
Kiromoni wilayani Bagamoyo hadi Mtoni Zanzibar.
No comments:
Post a Comment