Makadinali 142 kati ya 207 wanaotambuliwa na
Vatican wameshiriki ufunguzi wa mkutano mkuu mjini Vatican jana, kwa ajili ya
maandalizi ya kumpata mrithi wa Papa Benedict XVI.
Mkutano huo unafanyika Makao Makuu ya Kanisa Vatican, kwa ajili ya
maandalizi ya kumpata Papa wa 265, makadinali 103 wanaoruhusiwa kupiga kura
wakiwa tayari wapo mjini hapa, huku wengine 12 wakiwa njiani kuelekea Kanisa
Kuu la Mtakatifu Peter.
Wengi miongoni mwa waliokuwa wakisubiriwa, walitarajiwa kuwasili kuanzia jana mchana hadi asubuhi ya leo kwa ajili ya kuungana na wenzao.
Kwa mujibu wa msemaji wa Vatican, Padri Federico Lombardi,
makadinali waliokuwa wanatarajiwa kuwasili ni Naguib, Rai, Meisner, Rouco
Varela, Pham, Grocholweski, Sarr, Nycz, Woelki, Tong, Duka, Lehmann na Tong.
Idadi hiyo ya makadinali waliofanikiwa kwa wakati ni ya kwanza kuwahi
kufikiwa kwa siku ya kwanza, Lombardi alisema kwamba mkusanyiko huo mkuu
unafanyika kwa nidhamu ya hali ya juu na ushirika wa kiroho.
Kwa mujibu wa hotuba iliyotolewa na Msimamizi Mkuu na Mlezi wa
Makadinali, Angelo Sodano alisema mkusanyiko huo umejaa roho mtakatifu.
Kama inavyoelezwa na kifungu cha 12 ca Katiba ya Kitume inayosimamia
uchaguzi wa kipapa, makadinali hao watasomewa sehemu ya kwanza ya kiapo kwa
ajili ya uchaguzi wa Baba Mtakatifu kwenye Kitabu cha Injili, kuwekwa chini ya
msalaba na kiapo hicho kuwekwa muhuri.
Uchaguzi huo utafanyika katika 'mkutano fulani' kwanza, ulinajumuisha
wawakilishi watatu, ambao watasaidia katika serikali ya Kanisa kwa muda wa siku
tatu.
Katika nafasi aliyopewa jana alasiri, na mhubiri wa Kaya ya Kipapa,
Raniero Cantalamessa ataongoza kila kitu.
Mlezi huyo pia amependekeza Usharika kutuma ujumbe kwa Emeritus Papa
Benedict XVI, ambao ulikuwa na tatu mfupi, hatua zinazolenga shirika ya siku
Lombardi alihitimisha.
No comments:
Post a Comment