Language

Tuesday, 5 March 2013

HABARI ZA UCHAGUZI MKUU KENYA: UHURU KENYATTA BADO ANAONGOZA KWA KURA


Baada ya siku ndefu ya watu kupiga kura nchini Kenya, wengi wana hamu kujua rasmi mshindi wa uchaguzi wa urais. Hata hivyo matokeo ya mwanzo yameanza kutolewa na tume ya uchaguzi na mipaka Kenya, IEBC.


Matokeo hadi kufikia saa kumi na mbili jioni yalikuwa yanaonyesha Uhuru Kenyatta akiongoza dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga. Matokeo kutoka sehemu mbali mbali yalichelewa hasa kwa sababu ya hitilafu za kimitambo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...