Vichwa Vya Habari
Language
Tuesday, 23 April 2013
UNATAKA KUTUMA MAOMBI YA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU TCU? SOMA HAPA UJUE JINSI YA KUJIUNGA
Unaweza kutumia Internet au Simu yako ya mkononi. Soma kwa makini
maelekezo hayo muhimu kisha kuna link mwisho itakupeleka kwenye fomu za
kujisajili baada ya kuwa umeelewa cha kufanya.
Applications shall be made using one of the two ways, namely, Internet
and SMS applications. Applicants should not submit their applications to TCU or
NACTE by e-mail, fax, or deliver them in person.
Application through Internet 10.1.1 Holders of Tanzanian
certificates applying through the Internet should go through the
following steps:
following steps:
Labels:
HABARI MUHIMU
HABARI KUBWA ZA APRILI 22 NA 23 KWA UFUPI
Boston attack motive still unclear Monday, April 22, 2013
11:34:02 PM
The motive for the Boston Marathon bombing remains unclear, after prosecutors charged the surviving suspect in hospital.
The motive for the Boston Marathon bombing remains unclear, after prosecutors charged the surviving suspect in hospital.
Explosion at French embassy in Libya Tuesday, April 23,
2013 12:21:52 AM
A car bomb explodes outside the French embassy in the Libyan capital, Tripoli, wounding two guards and causing extensive damage, officials say.
A car bomb explodes outside the French embassy in the Libyan capital, Tripoli, wounding two guards and causing extensive damage, officials say.
Japan warns China on islands landing Tuesday, April 23,
2013 12:19:39 AM
Japan would respond with force if any attempt is made to land on disputed islands, PM Shinzo Abe warns, as eight Chinese ships sail in the area.
Japan would respond with force if any attempt is made to land on disputed islands, PM Shinzo Abe warns, as eight Chinese ships sail in the area.
Labels:
HABARI KWA UFUPI
MAREKANI YASHINIKIZA MAZUNGUMZO YA AMANI MASHARIKI YA KATI
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani John Kerry yuko mjini Brussels
ambako anatarajiwa kukutana na mkuu wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Jose
Manuel Barosso, na Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi Sergei Lavrov.
Kerry mwishoni mwa wiki alifanya ziara katika Ukingo wa Magharibi
katika juhudi za kushinikiza kuanzishwa tena mazungumzo ya amani kati ya Israel
na Palestina. Bruce Amani ana mengi zaidi
Akiwa mjini Istanbul hapo jana Jumapili, waziri huyo wa Mambo ya Kigeni
wa Marekani John Kerry alimtaka Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan
kuchelewesha ziara yake katika Ukanda wa Gaza mnamo Mei 16 baada ya kuitembelea
Ikulu ya Marekani, kwa sababu itahujumu juhudi za kuimarisha mahusiano baina ya
Uturuki na Israel.
Labels:
HABARI MUHIMU
Monday, 22 April 2013
VAN PERSIE NA USHINDI WA 20 WA MANCHESTER UNITED
Manchester United imetwaa rasmi ubingwa wa 20 wa taji la ligi kuu
soka nchini England kwa ushindi wa mabao matatu ya aina yake dhidi ya
Aston Villa,Mabao yaliyofungwa kwa ustadi mkubwa na mshambuliaji wa
kimataifa wa Uholanzi Robin Van Persie ambaye sasa atakuwa akiongoza
safu ya wafungaji kwa kufikisha mabao 24 huku Luis Suarez akifuatia
akiwa na mabao 23.
Van
Persie alifunga mabao yote matatu ndani ya dakika 31 za kipindi cha
kwanza katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Old Traford na
kuwafanya United kufikisha pointi tofauti ya 16 na waliokuwa mabingwa
watetezi majirani zao Manchester City,huku wakiwa na michezo minne
kibindoni.
Mkongwe Ryan Giggs alianza kwa kumtengenezea
nafasi ya goli la kwanza Van Persie dakika mbili baada ya mchezo kuanza
kabla ya Wayne Rooney kumpa nafasi nyingine nzuri Van Persie dakika ya
13 na kufunga moja kati ya mabao bora kabisa msimu huu kwa mguu wake wa
kushoto na kufanya United kuwa mbele kwa mabao mawili ndani ya dakika 15
za kwanza za mchezo.
Labels:
MICHEZO
MANCHESTER UNITED KUTANGAZA UBINGWA LEO IWAPO ITASHINDA LEO DHIDI ASTON VILLA
Ligi kuu ya soka nchini England itaendelea tena jumatatu ya leo kwa
mchezo mmoja kati ya Manchester United watakaokuwa nyumbani kwenye uwanja wa
Old Traford kuwakaribisha Aston Villa.
Mchezo huo ambao Manchester United inahitaji ipate ushindi
kujihakikisha ubingwa wa 20 wa ligi kuu soka nchini England na kuweka rekodi
mpya ya kuwa timu iliyochukua taji hilo mara nyingi zaidi ya Liverpool ambayo
ilikuwa inashikilia rekodi ya mataji 19.
United inakwenda kwenye mchezo huo ikiwa imetoka kulazimishwa sare ya
2-2 na West Ham United katika mchezo wa jumatano iliyopita. Aston Villa wao
watashuka uwanjani kucheza mchezo huo usiku wa leo wakiwa kwenye harakati za
kuepuka kushuka daraja la ligi kuu.
United katika michezo mitano iliyopita waliyocheza wamefungwa michezo
miwili,wameshinda miwili na kutoka sare mmoja huku Aston Villa katika michezo
mitano iliyopita waliyocheza wamefungwa mchezo mmoja na kushinda michezo mitatu
na kutoka sare moja dhidi ya Fulham.
Huu utakuwa mchezo wa 34 kwa timu zote kwenye ligi kuu soka nchini
Uingereza msimu huu ambapo zitakuwa zimebakisha michezo mingine minne kumaliza
ligi.
United wanaongoza ligi wakiwa na point 81 huku wakifuatiwa na watani
zao wa wajadi Manchester City ambao walifungwa hapo jana jumapili na Tottenham
kwa mabao 3-1,hivyo mchezo wa leo utaweza kuwafanya United wacheze kwa uhuru
zaidi na kutaka kujipa matumaini ya kuwavua rasmi ubingwa majirani zao
Manchester City. Aston Villa inayofundishwa na Paul Lambert inashika nafasi ya
17 wakiwa na point 34,pointi tatu zaidi ya Wigan wenye pointi 31 wakiwa kwenye
nafasi ya 18 ambayo ni kwenye kundi la timu tatu za mwisho zilizoko kwenye hatihati
ya kushuka daraja.
Aston Villa katika michezo 32 iliyopita waliyocheza na Manchester
United wameshinda mchezo mmoja,hiyo ilikuwa mwaka 2009 mwezi disemba pale Gabby
Agbonlahor alipofunga bao la kichwa kwenye uwanja wa Old Traford. Kwa upande wa
United, wao katika michezo 34 iliyopita ya ligi kuu tangu mwaka 1995 wamepoteza
mara moja tu dhidi ya Villa.
Wayne Rooney anatarajia kufikisha mchezo wake wa 400 akiwa na
Manchester United huku akiwa ameifungia klabu yake mabao tisa ya ligi kuu dhidi
ya Aston Villa ikiwa ni rekodi nzuri kwake kuifunga timu moja idadi kubwa ya
magoli,akiwa amezifunga idadi hiyo hivyo timu za Bolton, Fulham and Newcastle.
Labels:
MICHEZO
Sunday, 21 April 2013
WATU 185 WAPOTEZA MAISHA KATIKA MAPIGANO YA VIKUNDI VYA KIISLAMU NIGERIA
Mapigano ya wapiganaji wa kiislamu na vikosi vya usalama nchini Nigeria
yameripotiwa kutokea tangu usiku wa Ijumaa na kuendelea kwa muda mrefu ambapo
jumla ya watu 185 wanaripotiwa kufariki dunia katika mapigano hayo yaliyotokea
Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Serikali ya mji wa Baga na
Ofisa Serikali hiyo Bwana Lawan Kole.
Inasemekana kuwa watu wengi zaidi wamefariki dunia ambapo bado juhudi
za kutafuta maiti nyingine zinaendelea. Brigedia Jenarali Austin Edokpaye
amewaambia maafisa wakuu wa serikali kuwa,wapiganaji walitumia silaha kali na
maroketi yenye mabomu mazito kupambana na vikosi vya jeshi.
Aidha bwana Edokpaye aliongeza kuwa,wapiganaji hao walikuwa wakitumia
raia kama kinga yao kwa kujibanza karibu na makazi ya watu ambapo walijua vikosi
vya jeshi visingeweza kujibu mapigo.
Labels:
HABARI MUHIMU
Subscribe to:
Posts (Atom)





