Language

Wednesday 16 January 2013

MICHEZO: EMMANUEL OKWI AIAGA RASMI SIMBA SC

SHAMBULIAJI wa Simba SC, Mganda Emmanuel Okwi ameuzwa klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia kwa dola za Kimarekani 300,000.
 

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema mida hii kwamba, Okwi amekamilisha vipimo na kila kitu na tayari amesaini mkataba.
“Tunasubiri kulipwa fedha zetu tu, viongozi watakwenda Tunisia kuchukua fedha za mauzo ya mchezaji huyo,”alisema Poppe.
Okwi amekuwa akipiga chenga kuripoti kambini Simba SC na alikuwa hata hapokei simu za viongozi wa klabu hiyo kila alipopigiwa.
Kufuatia hatua hiyo, uongozi ulimuengua kwenye programu ya safari ya Oman na sasa inabainika ametua Sahel.
Baada ya kumaliza mkataba wake wa awali, Desemba mwaka jana aliongeza mkataba wa miaka miwili na Simba SC ambao kabla hajaanza kuutumikia, anahamia Sahel.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...