Language

Thursday 21 March 2013

BURUDANI: KAMA HUJAIPATA NGOMA MPYA YA DRAKE-STARTED FROM THE BOTTOM ICHUKUE HAPA

BURUDANI: UGAIDI WAMPELEKA JELA MIAKA 5 STAA WA MOVIE ZA KIHINDI (BOLLYWOOD) SANJAY DUTT



Mahakama ya juu kabisa nchini India leo imemhukumu mwigizaji filamu za Kihindi maarufu kama Bollywood, Sanjay Dutt, kifungo cha miaka mitano gerezani kwa kupatikana na silaha ambazo zilikuwa sehemu ya shehena ya silaha zilizotumiwa katika shambulio la mjini Mumbai mwaka wa 1993.

Mahakama hiyo ilishikilia hukumu ya Dutt iliyotolewa na mahakama ya kupambana na ugaidi mwaka wa 2007, lakini ikapunguza kifungo chake cha miaka sita. Mahakama hiyo ya juu kabisa India pia imeshikilia hukumu ya kifo iliyotolewa kwa Yakub Abdul Razzak Memon, kaka yake mshukiwa aliyepanga mashambulio hayo, Tiger Memon, na kubadilisha hukumu za kifo dhidi ya watu kumi kuwa kifungo cha maisha gerezani kufuatia shambulizi hilo. Maafisa wa ujasusi wanasema Tiger Memon pamoja na mshukiwa mwingine Dawood Ibrahim, ndio waliopanga shambulizi hilo, na bado wako mafichoni, wakiaminika kujificha nchini Pakistan. Milipuko ya bomu iliyapiga maeneo 13 mjini Mumbai, ikiwa ni pamoja na jengo kuu la soko la hisa, hoteli tatu na masoko kadhaa yenye shughuli nyingi, mnamo Machi 12 mwaka wa 1993, na kuwauwa watu 257. Watu wengine 800 walijeruhiwa.

BURUDANI: LISTEN OR DOWNLOAD NEW SONG RIVERSIDE-J-TONE

HABARI PICHA: NYOTA BONGO MOVIE YUSUPH MLELA


HABARI MUHIMU: MASHUA ILIYOBEBA 160 IMEZAMA NIGERIA


Mashua iliyokuwa imebeba watu 160 imezama umbali wa kilometa 74 toka pwani ya Nigeria, wanaosimamia shughuli za uokoaji wamesema.

Mashua hiyo, iliyoundwa kwa mbao, ilianzia safari yake huko kusini-mashariki mwa Nigeria Ijumaa, ikielekea Gabon, safari kati ya Afrika Magharibi na Kati inayopendwa na wafanyibiasahara wengi.
Tomi Oladipo wa BCC, akiwa mjini Lagos, anasema kwamba safari hizi huchukua siku kadhaa, na huwa si salama sana. Kwa ajili hiyo ajali hutokea mara kwa mara.
Mashua hiyo ilianzia safari mjini Oron, jimboni Cross River, na ilikuwa inasafiri katika Ghuba la Guinea ilipozama, duru rasmi zimesema.

HABARI KWA UFUPI: HIZI NDIO HABARI ZILIZOTAWALA KWENYE VYOMBO VINGI VYA HABARI LEO KWA UFUPI

Kurd rebel leader calls Turkey truce Thursday, March 21, 2013 4:19:21 PM
The jailed leader of Kurdish rebels, Abdullah Ocalan, calls a ceasefire and urges his fighters to withdraw from Turkey after years of war.
Obama vows Palestinian state support Thursday, March 21, 2013 4:21:05 PM
President Barack Obama says the US is "deeply committed" to the creation of an independent Palestinian state during a visit to the West Bank.
Cyprus 'scraps bank levy' - new plan Thursday, March 21, 2013 3:52:13 PM
Cyprus has apparently dropped an unpopular levy on bank deposits, in an emerging new plan to secure a huge international bailout.

HABARI MUHIMU: MVUA YAUA 27 BRAZIL


Takriban watu 27 wamefariki baada ya ardhi kuporomoka mjini Petropolis, eneo la milimani kaskazini mwa Rio de Janeiro, Brazil, baada ya mvua kubwa kunyesha.


Maporomoko hayo ya ardhi yaliukumba mji wa Petropolis baada ya mto kufurika.
Kundi kutoka Brazilian National Force limetumwa eneoni ili kuwasaidia waokoaji.

MICHEZO: RATIBA YA MECHI KUBWA ZA LEO


HABARI MUHIMU: ALIYEMGONGA TRAFIKI KUFIKISHWA KORTINI MUDA WOWOTE KUANZIA SASA


Dereva wa gari lililomgonga na kumuua askari wa usalama barabarani, Elikiza Nko atafikishwa kortini wakati wowote baada ya upelelezi kukamilika, ilielezwa jana.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini(trafiki), Mohammed Mpinga alisema hayo jana alipozungumzia tukio hilo ambalo lilisababisha simanzi kwa watu wengi.
Mpinga alisema polisi walifanikiwa kumkamata mhusika kwa mbinu za kipolisi na kwamba kwa jana alikuwa akihojiwa ili kupata ushahidi utakaowezesha kumpeleka kortini.
Alisema dereva huyo ni kati ya wale wawili waliowakamata   awali na  hatimaye mmoja walimbaini kuwa ni mhusika .

HABARI MUHIMU: TUME YA PINDA YAELEKEA KUPATA SABABU KUU ILIYOFELISHA WANAFUNZI KIDATO CHA NNE


Ukosefu wa walimu, upungufu wa vitabu na mazingira duni ya kujifunzia, ni baadhi ya sababu zilizotolewa kwa wingi na wadau wa elimu waliohojiwa na Tume ya Kuchunguza Matokeo ya Kidato cha Nne mwaka 2012 iliyoundwa na Waziri Mkuu.

Hayo yalielezwa jana na Mwenyekiti wa tume hiyo, Profesa Sifuni Mchome alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
“Watu wengi wanasema sababu za matokeo kuwa mabaya ni shida ya walimu, vitabu vichache na vingine vimepitwa na wakati, wanazungumzia pia usimamiaji wa shule na ukaguzi,” alisema Profesa Mchome.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...