Language

Thursday 17 January 2013

HABARI: TIGO IMEGOMA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UPIGAJI SIMU

Naibu Mkurugenzi wa Utekelezaji wa Kanda wa TCRA, Victor Nkya, alisema punguzo hilo ni la kutoka asilimia 35 hadi asilimia 69 na kwamba litaanza kutumika Machi mosi mwaka huu
.WAKATI Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwasilisha rai ya kupunguza gharama za mwingiliano wa simu , Kampuni ya Tigo imekataa kufanya hivyo kwa madai kuwa itahatarisha uwekezaji wake kwa punguzo la asilimia 69.



Msimamo huo wa Tigo, umekuja baada ya TCRA kukutana na wadau wa mawasiliano jana jijini Dar es salaam, ili kukusanya maoni kuhusu mapendekezo ya kupunguza gharama ya mtandao mmoja kwenda mwingine. Hatua hiyo inalenga katika kuwasaidia wananchi kumudu gharama za mawasiliano ya simu.

Naibu Mkurugenzi wa Utekelezaji wa Kanda wa TCRA, Victor Nkya, alisema punguzo hilo ni la kutoka asilimia 35 hadi asilimia 69 na kwamba litaanza kutumika Machi mosi mwaka huu na kukoma Desemba 31 mwaka 2017 .

Nkya alisema punguzo la gharama ya kupiga mtandao mmoja kwenda mwingine kwa mwaka 2013 litakuwa asilimia 34.92, mwaka 2014 asilimia 32.40, mwaka 2015 asilimia 30.18, mwaka 2016 asilimia 28.57 na mwaka 2017 ni asilimia 26.96.
“Lengo letu ni kupunguza gharama za mwingiliano wa simu, mfano mwananchi ambaye yupo Tigo anapiga kwenye mtandao wa Vodacom hizi gharama atazilipa mwenye kampuni ya Vodacom kuilipa kampuni ya Tigo badala ya kulipa mwananchi kama ilivyo sasa,” alisema.
Alisema maoni yanayotolewa na wadau yatachukuliwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mawasiliano na kuyafanyia kazi.
Ofisa Mdhibiti wa Kampuni ya Tigo, Levocatus Nkata, alisema punguzo hilo ni kubwa hivyo wawekezaji watashindwa kuendesha kampuni zao.
Alisema Kampuni ya Tigo inatoa huduma zake hadi vijijini na kwamba hatua hiyo itaifanya ishindwe kupeleka na kutoa huduma kwenye maeneo hayo.
Nkata alisema itachukua muda mrefu kurudisha gharama walizotumia kuendeshea kampuni yao kutokana bei ya kuendesha mitambo.
“Sisi hatukubaliani na hayo mapendekezo yaliyoletwa na TCRA, punguzo hilo kwa sisi wawekezaji ni kubwa sana, tunachoomba wasipunguze ibaki kama ilivyo na kwa mwaka 2017 tunaomba ipunguze kufikia asilimia 45 tu, “alisema Nkata.
Kampuni za Airtel, Vodacom , Benson na Dovetel zimekubali punguzo hilo lakini zimeiomba TCRA ipunguze asilimia chache.

MICHEZO: SUAREZ AKIRI KUJIANGUSHA KATIKA MEHI DHIDI YA STOKE CITY


 Luis Suarez

Msambulizi wa liverpool, Luis Suarez, ana amini kuwa analengwa sana na vyombo vya habari vya Uingereza lakini amekiri alijiangusha katika mechi moja ya ligi kuu msimu huu.

Katika mahojiana na kituo kimoja cha habari cha ametika ya kusini, mshambulizi huyo kutoka Uruguay, amesema kila mara yeye huangaziwa pakubwa na mashirika hayo kwa kuwa jina lake linafanya magazeti kuuza zaidi.
Suarez ambaye ndiye mfungaji bora wa liverpool msimu huu huku akiwa amefunga magoli 15, mawili nyuma ya nyota wa manchester United Robin van Persie, amekiri alijiangusha wakati wa mechi yao na Stoke City tarehe saba October mwaka uliopita.
Tangazo hilo la suarez limemuudhi kocha wa liverpool brendan roggers, ambaye amesema, mchezaji huyo ataadhibiw kuambatana na sheria za klabu hiyo.
Roggers, ametaja tangazo hilo la Suarez, kama moja ambalo kamwe halikubaliki.

MICHEZO: PEP GUARDIOLA AMWAGA WINO BAYERN MUNICH MIAKA 3



Pep Guardiola, mwenye umri wa miaka 41, awali ilidhaniwa angelijiunga na Chelsea, au Manchester City, zote za Uingereza.


Guardiola ametia saini mkataba wa miaka mitatu na Bayern Munich, hadi mwaka 2016.
Atachukua madaraka ya Jupp Heynckes, ambaye ameamua kustaafu.
Siku zake akiwa mchezaji, Guardiola, aliwahi kuvichezea vilabu vya Barcelona, Brescia, Roma, Al.-Ahli, Dorados na pia timu ya taifa ya Uhispania.
Alikabidhiwa pia tuzo nyingi akiwa mchezaji.
Katika kazi ya meneja, amewahi kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Uhispania, La Liga, mara tatu, ushindi wa Supercopa de Espana mara tatu, mara mbili kutwaa ubingwa wa Copa Del Rey, ubingwa mara mbili wa klabu bingwa barani Ulaya, mara mbili Kombe la Uefa na vile vile mara mbili ubingwa wa Kombe la Dunia la FIFA kwa upande wa vilabu.
Guardiola, ambaye alizaliwa tarehe 18 Januari, mwaka 1971, Santpedor, Uhispania, tangu kuondoka uwanja wa Nou Camp mwezi Mei mwaka 2012, amepumzika msimu mzima, baada ya kukiwezesha klabu kupata jumla ya vikombe 14, ikiwa ni pamoja na ushindi wa klabu bingwa barani Ulaya mara mbili.

HABARI: WANAJESHI 200 WA NIGERIA KWENDA KUONGEZA NGUVU MALI

Takriban wanajeshi 200 wa Nigeria wanatarajiwa kuwasili nchini Mali kusaidia katika harakati dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu Kaskazini mwa nchi.

 

Ni kikosi cha kwanza cha jeshi kutoka Magharibi mwa Afrika kujiunga na wanajeshi wa Ufaransa walioanza kupambana na wapiganaji wa kiisilamu tangu Ijumaa iliyopita.
Wakati huohuo, wanajeshi wa Mali na Ufaransa, wameanza operesheni yao ya ardhini dhidi ya wapiganaji hao wa kiisilamu.
Duru zinasema kuwa makabiliano yalizuka kati ya waasi na wanajeshi mjini Diabaly, umbali wa kilomita 350 kaskazini mwa mji mkuu Bamako siku ya Jumatano.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...