Language

Friday 29 March 2013

SAUTI SOL KATIKA TUZO ZA KIMATAIFA ZA UANDISHI BORA

Kundi maarufu la muziki nchini Kenya Sauti Sol ni wasanii pekee ambao wako  katika Tuzo za kimataifa za Waandishi bora wa Nyimbo.
 

HABARI KUBWA ZA LEO KWA UFUPI


N Korea 'readies rocket force' Thursday, March 28, 2013 10:30:42 PM
North Korea says it has put missile units on stand-by to attack US targets in response to US stealth bomber flights over the Korean peninsula.
Zuma reassures S Africa over Mandela Thursday, March 28, 2013 12:19:07 PM
President Jacob Zuma says South Africans "must not panic" as ex-leader Nelson Mandela undergoes treatment for the recurrence of a lung infection.
Spacecraft shortens trip to ISS Thursday, March 28, 2013 11:57:48 PM
A Soyuz space capsule docks at the International Space Station (ISS) after a journey of under six hours - much shorter than the normal two-day flight.

LWAKATARE WA CHADEMA APANGIWA JAJI MPYA


Maombi ya Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare kupinga utaratibu wa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kumfutia mashtaka kisha kumkamata na kumfungulia tena mengine, tayari yamepangiwa jaji wa kuyasikiliza.

Habari zilizopatikana jana na kuthibitishwa na mmoja wa mawakili wanaomtetea Lwakatare, zinadai maombi hayo yamepangwa kusikilizwa na Jaji Lawrence Kaduri. Hata hivyo, tarehe ya kusikilizwa kwa maombi hayo haijapangwa.
Lwakatare anayekabiliwa na kesi ya ugaidi na mwenzake Ludovick Joseph, kupitia kwa jopo la mawakili wanaomtetea, wiki iliyopita aliwasilisha maombi Mahakama Kuu Dar es Salaam akipinga uamuzi wa DPP kuwafutia mashtaka kisha kuwakamata na kuwafungulia tena mashtaka hayo.

MANDELA HOSPITALINI TENA


Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amelazwa tena hospitalini baada ya kuugua ugonjwa wa mapafu kwa mara nyingine.

Taarifa kutoka kwa serikali ya nchi hiyo, ilisema kuwa Mandela mwenye umri wa miaka 94 alilazwa hospitalini muda mfupi kabla ya saa sita usiku.
Mandela alilazwa siku kumi na nane hospitalini mwezi Disemba mwaka jana kupokea matibabu ya ugonjwa wa mapafu na kibofu.
Anasifika sana kama baba wa taifa hilo kwa kuongoza vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.
Kadhalika Mandela alihudumu kama rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini tangu mwaka 1994 hadi mwaka 1999, ingawa hali yake ya kiafya imezua wasiwasi kwa muda sasa.
Rais Jacob Zuma alimtumia taarifa ya kumpa pole na kumtakia kupona Mandela
"tunawataka watu wa Afrika Kusini pamoja na duniani kote kuwa watulivu na kumuombea Madiba na familia yake. Tuna imani kuwa kikosi cha madaktari wanaomtibu Mandela watafanya kila hali kuhakikisha anapona,'' alisema Zuma katika taarifa yake.
Mapema mwezi huu bwana Mandela alilazwa hospitalini mjini Pretoria baada ya kufanyiwa ukaguzi wa kiafya.

SIMANZI LATAWALA MSIBANI KWA MBUNGE WA CUF, MAKINDA AFIKA KUTOA POLE NA MWILI WA MAREHEMU KUPELEKWA PEMBA


Mbunge wa Chambani (CUF), Salim Hemed Khamis (60) amefariki dunia jana katika hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa baada ya kuanguka ghafla juzi kwenye Ofisi za Bunge, Dar es Salaam.

Kifo cha mbunge huyo kimewagusa wengi akiwamo Rais Jakaya Kikwete ambaye ametoa ndege yake ili kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Pemba. Ofisi ya Bunge imethibitisha kutokea kwa kifo hicho cha mbunge huyo na kueleza kuwa, alipatwa na ugonjwa wa kiharusi uliosababishwa na ugonjwa wa moyo (Hypertension).

Khamis anatarajiwa kusafirishwa kisha kuzikwa leo kijijini kwao Chambani, Pemba baada ya jitihada za kumsafirisha jana kushindikana na wabunge wengi kuomba kushiriki kumuaga.
Mbunge huyo atasafirishwa leo saa tatu asubuhi baada ya shughuli ya kuaga itakayofanyika kwenye Viwanja vya Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Spika wa Bunge, Anne Makinda ametangaza kusitishwa kwa shughuli zote za Kamati za Bunge hadi Jumanne Aprili 2, kutokana na msiba huo.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Makinda alisema: “Ninatoa pole kwa familia ya marehemu, wananchi wa Chambani, Wajumbe wa Kamati ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, wabunge wote na Watanzania wote kwa jumla”.

MSIMAMO WA LIGI KUU YA UINGEREZA (EPL)


RATIBA YA MECHI MBALI MBALI ZA LEO


NYOTA WA BONGO MOVIE ROSE NDAUKA


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...