Language

Friday 29 March 2013

SAUTI SOL KATIKA TUZO ZA KIMATAIFA ZA UANDISHI BORA

Kundi maarufu la muziki nchini Kenya Sauti Sol ni wasanii pekee ambao wako  katika Tuzo za kimataifa za Waandishi bora wa Nyimbo.
 
Kundi hilo linaloundwa na wasanii wa 4 wote wakiwa ni wanaume wameingia katika mashindano hayo ambayo mshindi atatangazwa mwezi April kuptia wimbo wao unaoitwa 'Soma Kijana'.
Mashindano hayo unaandishi bora wa nyimbo ni moja ya mashindano yanayoheshimika duniani, hivyo litakuwa na changamoto ya kupambana na wasanii wengine kutoka sehemu zote duniani ambao walifanikiwa kuchaguliwa kwenye fainali hizo.
Baadhi ya majaji katika mashindano hayo ni Nas, Elton John, Janelle Monae, Devo na Anthony Hamilton.
Kundi la Saut Sol limepata umaarufu hapa nchini baada ya wimbo ambao walishirikishwa na Ay unaoitwa 'Don't wanna be alone' kufanya vizuri.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...