Language

Thursday 25 April 2013

TUKIO LA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR KATIKA PICHA


MATOKEO YA MECHI ZILIZOCHEZWA APRILI 25


UNAMFAHAMU ALIYEBUNI JINA LA TANZANIA? MSOME HAPA


HISTORIA ya Tanzania haiwezi kukamilika bila kutaja jina la mtu maarufu aliyebuni jina la Tanzania ambaye kwa bahati mbaya au kwa makusudi hakumbukwi tena.


Tunaelezwa kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lakini nani kati yetu amekuwa akijiuliza jina la Tanzania lilivyopatikana na nani hasa alilibuni?
Wengi tunaambiwa kuwa jina la Tanzania lilipendekezwa na Watanganyika, Wazanzibari na raia wengine wa nje lakini hawatajwi waziwazi na picha zao tukaziona.
Inaaminika kuwa mtu aliyebuni jina la Tanzania ni MOHAMMED IQBAL DAR, raia wa India ambaye alikuwa miongoni mwa watu walioshindana katika shindano la kubuni jina la nchi mpya baada ya Tanganyika na Zanzibar kuungana.
Mohammed alizaliwa mkoani Tanga miaka ya 1944; baba mzazi wa Mohammed alikuwa daktari huko mkoani Morogoro akiitwa Dk. T . A DAR aliyefika Tanganyika kuanzia mwaka 1930.
Mohammed Iqbal Dar alipata elimu yake ya msingi mkoani Morogoro katika Shule ya Msingi H. H D Agakhan ambayo kwa sasa ni mali ya serikali. Alijiunga na Shule ya Sekondari Mzumbe alikosoma kidato cha kwanza hadi cha sita.

BRAZIL KUONGEZA NGUVU KATIKA KIKOSI DRC

Umoja wa Mataifa umemteua Generali mmoja raia wa Brazil ambaye anasifika kwa kudhibiti mtaa mmoja wa mabanda nchini Haiti kutokanamana na vurugu kuweza kuwaongoza walinda amani wa Umoja wa Mataifa katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Generali Carlos Alberto dos Santos Cruz ataongoza kikosi cha wanajeshi 20,000, ikiwemo kikosi kipya cha wanajeshi kitakachopambana na waasi mashariki mwa nchi.
Hii ndio mara ya kwanza kwa Umoja wa mataifa kukabidhi kikosi cha wanajeshi nguvu kuweza kupambana na waasi.
Generali Santos Cruz, aliambia BBC kuwa wanajeshi wake, watafunzwa namna watakavyo pambana na waasi bila kuwajeruhi raia na kuharibu mali nchini Congo.
"eneo tete zaidi siku hizi ni Mashariki mwa nchi,'' Cruz alimbia BBC
"niko tayari kukabiliana, na hali ngumu zaidi. Lengo kuu ni kuwaondolea hali ngumu wanayokabiliana nayo watu wa Congo.''

KURA ZA MAONI KUPIGWA JUU YA AMANI NCHINI MALI


Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupigia kura azimio linalopendekeza kuundwa kwa kikosi cha kulinda amani nchini Mali.

Kikosi hicho chenye wanajeshi 12,600 kinajumuisha takriban wanajeshi 6,000 kutoka nchi za Magharibi mwa Afrika ambazo tayari zina wanajeshi wao nchini humo.
Azimio hilo limependekezwa na Ufaransa ambayo iliingilia kati mzozo wa Mali mnamo mwezi Januari ili kupambana na wapiganaji wa kiisilamu Kaskazini mwa nchi hiyo.
Kikosi hicho kinatarajiwa kwenda Mali mwanzoni mwa mwezi Julai kabla ya uchaguzi mkuu.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...