Language

Friday 11 January 2013

BURUDANI: HIVI UNAJUA JACKLINE WOLPER HAJALIPA MIL. 16 ALIZOTOA MSAADA KWA SAJUKI? FULL STORY IKO HAPA

Kama unakumbuka msanii Jackline Wolper alimpatia sh mil 16 Sajuki kwa ajili ya matibabu nchini India, sasa yameanza kuibuka mengine ambapo inadaiwa kuwa kiasi hicho cha fedha alichukua kwa mtu na mwenye nazo ameshindwa kuvumilia ameamua kuanza kumdai ili azirudishe tofauti na makubaliano yalivyokuwa.

Inadaiwa kuwa habari hizo zilianza kuzuka tangu siku ambayo Sajuki amefariki, huku mwenye fedha hizo akidai kuwa alitoa fedha hizo kwa makubaliano kwamba atarudishiwa mapema lakini hadi muda waliopangwa umepita haoni dalili zozote za kupewa fedha zake.

Chanzo kimoja cha kuaminika kilizungumza na mwandishi wetu kutoa story ilivyo, ambapo kilidai kuwa ishu hiyo imeanza kujitokeza upya siku ya msiba na wenyewe walitaka kulipana kimya kimya lakini baada ya maneno kuwa makubwa wamepanga kulipana muda wowote sasa.

Hata hivyo chanzo hicho kilisema kuwa Wolper hakutakiwa kutoa kiasi chote cha pesa kwa Sajuki lakini alifanya hivyo ili kuonekana mbele za watu kuwa ndiye aliyefanya mambo makubwa wakati hamna kitu.

“Msibani maneno yalikuwa yanazungumzwa sana tena chini kwa chini mwenyewe Wolper kainamisha kichwa chini kwa aibu asa sijui atazilipa maana huyo mwenye nazo ni mbongo wa kawaida lakini si mtu wa njaa kama sisi bongo movie,”
alisema.

MICHEZO: HII NDIO RATIBA YA MECHI MBALI MBALI UINGEREZA NA UFARANSA


HABARI: MCHUNGAJI MTIKILA AFUFUA MAPYA KATIKA MCHAKATO WA KUTOA MAONI YA KATIBA MPYA


MAKUNDI maalumu jana yaliendelea kutoa maoni yao kwenye mchakato wa Katiba Mpya, huku DP kikipendekeza Rais aapishwe baada ya siku 90 tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu.
 Mbali na maoni hayo yaliyowasilishwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Mchungaji Christopher Mtikila, makundi mengine; wakulima, wafugaji, wanahabari na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) nayo yalijitokeza kutoa moyoni.Mtikila alisema kipindi hicho cha siku 90 kitatoa fursa kwa watu wanaotaka kuwasilishapingamizi dhidi ya ushindi wa Rais mteule kufanya hivyo, kabla ya kuapishwa.Alisema pingamizi linaweza kufanyiwa kazi kwa kipindi hicho cha miezi mitatu ili kuhakikisha kuwa taifa linapata kiongozi halali mwenye ridhaa ya wananchi.
“Pia tunataka kinga ya Rais ikome pale anapomaliza muda wake wa uongozi, kama alifanya makosa yoyote ya jinai aweze kushtakiwa ili kujenga nidhamu ya uongozi katika ofisi ya umma. Utaratibu wa kumwondoa madarakani uimarishwe asisubiriwe hadi amalize muda wake wa uongozi.”
Alisema kuwa Katiba ya nchi inapaswa kuwa mali ya wananchi wenyewe ili watawala wasijihusishe katika kuwaundia wananchi Katiba kama ilivyo kwa mchakato unaoendelea sasa wa kupata Katiba Mpya.
“Kumekuwa na hoja ya kuwapo kwa Serikali ya Tanganyika, hilo ni jambo muhimu na watu kutoka Tanganyika ni lazima wawe na Serikali yao ndani ya mipaka ya ardhi yao kupitia Katiba Mpya,” alisisitiza Mchungaji Mtikila.
Aliongeza kuwa nafasi za wabunge wa viti maalumu bungeni ziondolewe ili viti hivyo vishindaniwe kidemokrasia. Alisema wanawake wanatakiwa waelimishwe na kupikwa ili wahimili ushindani katika medani za kisiasa. Alisema kuwa taifa linahitaji viongozi bora na siyo kustarehesha jinsia.

BURUDANI:NYIMBO MPYA: SIKILIZA NA UDOWNLOAD 'LISTEN' YA BELLE 9 FREE MP3

BURUDANI:KALA JEREMIAH KUIACHIA PASAKA JUMAPILI


MICHEZO: NIGERIA KUSHINDA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA 2013?

Wacheza kamali wanataka kucheza karata zao vizuri kuhusu kinyang'anyiro cha ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013.

 
Wacheza kamali hao wataelekeza karata yao katika timu ya Nigeria wakiipa nafasi ya kuwa katika timu tatu bora za juu.

Timu ya Nigeria, The Super Eagles, imeshiriki mara 16 katika mashindano ya kombe hilo na kushinda mara mbili, ikishika nafasi ya pili mara nne na mara saba katika nafasi ya tatu, ikiwa ni rekodi ya kujivunia katika kipindi cha miaka 50.

UN YAOMBA MSAADA WA KIJESHI MALI


Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Susan Rice, alihoji ikiwa rais Dioncounda Traore alikuwa ametoa ombi maalum na kufafanua aina ya msaada anaotaka. 

Ufaransa inatarajiwa kutoa jibu lake leo wakati wa mkutano wa dharura utakaofanyika , kwa mujibu wa balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa, Gerard Araud.
Mwezi jana Umoja wa Mataifa uliidhinisha mpango wa kutuma wanajeshi elfu tatu kuweza kutwaa eneo la Kaskazini mwa nchi ambalo linadhibitiwa na makundi ya kigaidi yaliyo na uhusiano na kundi la Al Qaeda.
Wapiganaji wa kiisilamu wameweka sheria kali za kiisilamu katika eneo hilo.
Kwa sababu ya mipango ya usafiri na vifaa , kikosi cha wanajeshi wa Afrika hakitatarajiwa kuanza kazi hadi ifikapo Septemba au Oktoba

BURUDANI: TRACK MPYA NA KALI KULIKO YA THE BATO-GET UR BODY BUSY

Kama ulikuwa humjui ni kati ya jamaa waliokuja kasi katika game ya muziki wa bongo flava na pia ni mwana muziki mwenye nyimbo nyingine kali ambazo pia utazipata kupitia hapa hapa www.bonmusic5.blogspot.com iliyotengenezwa na producer Stevee wa STREET SOUND RECORDS.

BURUDANI: KAMA BADO HUJAISIKILIZA AU HUJAIPATA NYIMBO YA ROMA 2030 IKO HAPA, UNAWEZA KUISIKILIZA AU KUIDOWNLOAD

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...