Language

Thursday 21 March 2013

BURUDANI: UGAIDI WAMPELEKA JELA MIAKA 5 STAA WA MOVIE ZA KIHINDI (BOLLYWOOD) SANJAY DUTT



Mahakama ya juu kabisa nchini India leo imemhukumu mwigizaji filamu za Kihindi maarufu kama Bollywood, Sanjay Dutt, kifungo cha miaka mitano gerezani kwa kupatikana na silaha ambazo zilikuwa sehemu ya shehena ya silaha zilizotumiwa katika shambulio la mjini Mumbai mwaka wa 1993.

Mahakama hiyo ilishikilia hukumu ya Dutt iliyotolewa na mahakama ya kupambana na ugaidi mwaka wa 2007, lakini ikapunguza kifungo chake cha miaka sita. Mahakama hiyo ya juu kabisa India pia imeshikilia hukumu ya kifo iliyotolewa kwa Yakub Abdul Razzak Memon, kaka yake mshukiwa aliyepanga mashambulio hayo, Tiger Memon, na kubadilisha hukumu za kifo dhidi ya watu kumi kuwa kifungo cha maisha gerezani kufuatia shambulizi hilo. Maafisa wa ujasusi wanasema Tiger Memon pamoja na mshukiwa mwingine Dawood Ibrahim, ndio waliopanga shambulizi hilo, na bado wako mafichoni, wakiaminika kujificha nchini Pakistan. Milipuko ya bomu iliyapiga maeneo 13 mjini Mumbai, ikiwa ni pamoja na jengo kuu la soko la hisa, hoteli tatu na masoko kadhaa yenye shughuli nyingi, mnamo Machi 12 mwaka wa 1993, na kuwauwa watu 257. Watu wengine 800 walijeruhiwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...