Language

Tuesday 5 February 2013

HABARI MUHIMU: SASA NDOA ZA JINSIA MOJA RUKSA UINGEREZA

Jonathan Blake

Baada ya kusubiriwa kwa muda sasa, wanasiasa wa Uingereza wameupigia kura ya ndio muswada wa sheria ya ndoa za jinsia moja, ambapo katika bunge la nchi hiyo "House of Commons" wabunge 400 wameridhia, ilhali wabunge 175 wamepiga kura ya hapana.

Katika taarifa ambayo GK imefuatilia kupitia vyombo vya  habari vya kimataifa na kupitia maoni ya wakazi wa jiji la London, imeonekana kuwa wananchi wako katika pande mbili, baadhi wakionyesha kukerwa na hatua hiyo, wakati wengioneo wakionekana kutokuwa na shida kabisa.
Kwa ufupi ni kwamba kupitishwa kwake kutapelekea kurahisisha pia kwa watu wa jinsia mmoja kuasili watoto na kuwalea kama wazazi wa asili, jambo ambalo linatatajwa kuja kuwaathiri watoto hao baadae.
Vuta picha ya ulipokuwa mtoto na ukijiandaa kwenda shule kisha unawaaga wazazi wako, kwa hawa watoto wataitaje Mama na Baba?
katika hali ya kushangaza zaidi, katika mahojianoa ambayo yamemalizika hivi punde kupitia kituo cha shirika la utangazaji cha Uingereza, Askofu wa Greater London, Jonathan Clive Blake ameonekana kuunga mkono na kufurahia jambo hilo kupitishwa, akisema kwamba kila mtu ana haki ya kuoa na kuolewa, na kuwataka watu kutowabagua wananchi wenzao.
 
 Askofu Jonathan Blake
Kwa upande wake, muwakilishi wa muungano wa ndoa nchini humo, "Coallition for Marriages", Dr Sharon James amesema kuwa kitendo hicho sio cha kufurahia hata kidogo, kwani ni kinyume na maadili na hata kwa namna ambavyo utamaduni wa ndoa unatakiwa kuwa.
Waziri Mkuu, James Cameron ni mmojawapo wa wabunge waliopiga kura ya ndio kuafikiana na muswada huo, ambao hata hivyo umeonekana kukigawa chama chake cha Conservative kimtazamo.
Endelea kuwa na GK, na itakuhabarisha kadri ambavyo tutaendelea kupata taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...