MATUKIO ya kutisha na ya kinyama dhidi ya watoto wadogo yameendelea
kuutikisa Mkoa wa Mbeya, baada ya mwanafunzi wa chekechea, Ayoub Agen (6) kuuwa
kwa kuchinjwa mithili ya kuku na wauaji kuondoka na kichwa chake.
Hata hivyo wananchi wenye hasira walifanikiwa kumnasa mmoja wa
watuhumiwa wa tukio hilo, ambaye hata hivyo jina lake halikuweza kupatikana
ambapo baada ya kummbana ili aeleze sehemu walikokificha kichwa cha
marehemu aligoma hivyo kuamua kumteketeza kwa moto.

Akifafanua zaidi Mwenyekiti huyo alisema, marehemu Agen
alikuwa ni mwanafunzi wa chekechea katika shule ya msingi Lusanje kijijini hapo
na kwamba alikutwa na mauti hayo ya kikatili baada ya watu hao wasiofahamika
kufanikiwa kumuiba nyumbani kwao.
Mwaikenda alisema mwili wa marehemu uliokotwa ukiwa
umetenganishwa kichwa na kiwiliwili huku kichwa kikiwa hakionekani hadi sasa
ikiwa ni muda mfupi tu baada ya watu hao wasiofahamika kumwiba toka nyumbani
kwa wazazi wa marehemu .
Mkazi mwingine katika kijiji hicho, Tumpale Sankemwa, alikielezea mkasa
huo, alisema baada ya wananchi kugundua mwili huo wa marehemu waliendelea
kuwasaka wahusika na wakiwa katika harakati hizo ghafla walikutana na mtu mmoja
ambaye walimtilia mashaka.
Alisema baada ya kumfanyia mahojiano ya kina kwa kuwa alikuwa
hafahamiki na mgeni kijijini hapo, alikuwa akijibu jeuri hivyo kuwapandisha
hasira wananchi jambo lililosababisha kuanza kumshambulia na hatimaye kumuua
papo hapo.
Hata hivyo alisema wakati wananchi wakiendelea kumshushia kipigon mtu
huyo licha ya kutotaja jina lake, alikiri kuhusika katika tukio hilo kwa
kueleza kuwa waliohusika walikuwa watatu na kwamba wenzake walikuwa wameondoka.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Kamishina Msaidizi wa jeshi la
polisi,Diwani Athumani, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba hadi
sasa kichwa cha marehemu huyo hakijaonekana na jeshi hilo linaendelea
kufanya uchungu.
No comments:
Post a Comment