www.facebook.com/bonmusicblogLigi Kuu ya Vodacom inaendelea leo (Aprili 13 mwaka huu) kwa mechi mbili
zitakazochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, na Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sokoine jijini Mbeya.
Yanga itakuwa mwenyeji wa Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa wakati
Uwanja wa Sokoine utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Tanzania Prisons na Ruvu
Shooting.
Ligi hiyo itaendelea kesho (Aprili 14 mwaka huu) kwa mechi kati ya
wenyeji Azam na Simba. Mechi hiyo namba 155 itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment